Mshambuliaji wa Kimataifa wa Simba, Paul Kiongera, raia wa Kenya, amelazimika kuchelewa kupelekwa India kufanyiwa matibabu ya goti kufuatia kuwepo kwa sherehe za wiki ya Kiislamu inayojulikana kama Ashura.
Kiongera aliumia goti katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union ambapo katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 2-2.
Rais wa Simba, Evans Aveva, amesema Kiongera alitakiwa kuondoka nchini wiki iliyopita, lakini amecheleweshwa na sherehe za Kiisalamu ambapo nchini India wamekuwa katika pilikapilika hizo na kudai kuwa daktari aliyepewa jukumu hilo, ametaka apelekwe sherehe zitakapomalizika.
“Mikakati ya kumpeleka Kiongera bado ipo palepale, kwani taratibu zote zimeshafanywa na bajeti ambayo tumeipanga ni kuanzia Sh milioni 8.5 hadi 10, kwa ajili ya zoezi lote la kufanyiwa upasuaji.
“Alitakiwa aondoke nchini wiki hii lakini imeshindikana kufuatia uwepo wa sherehe za wiki ya Kiislamu ambapo daktari wake ametaka apelekwe mara baada ya kumalizika kwa tukio hilo na hatujajua atakaa muda gani huko,” alisema Aveva.
0 comments:
Post a Comment