Na Ben Shija, Dar es Salaam,
Mabadiliko
si ‘ kitu cha kuhesabu’, lakini mengi yanatokea. Yoote husababishwa na ‘
Kiu’, ikiwa Azam FC walikuwa na kiu ya kutwaa ubingwa wa kwanza wa
Tanzania Bara, Simba SC, Yanga SC wao pia walikuwa na kiu ya kutaka
kuongeza mafanikio zaidi ya ndani ya uwanja kwa ushindi wa mataji kila
msimu. Kiu si kitu cha kuburudika au kuondoka, Iliumbwa sababu ya Uhai,
na itaondoka sababu ya uhai. Kiu gani wanayo klabu kubwa kama Simba Sc?
Tuachane
na ukweli kuwa klabu hii ( Simba SC) ni mabingwa mara 19 wa Kihistoria
wa ligi kuu ya Bara, timu hiyo kwa sasa imekuwa na –u-haba’ wa mataji ya
ligi kuu na kile cha kusikitisha zaidi kwa wapenzi wa klabu hiyo ni
kukosa kuwa miongoni mwa klabu Mbili za juu kwa msimu mitatu mfululizo.
Kiuhalisia nafasi ya Simba hivi sasa imechukuliwa na Azam FC ambayo
ndani ya misimu minne mfululizo timu hiyo ya Chamanzi imemaliza namba 2
mara tatu na mara moja wamefanikiwa kushinda ubingwa.
Siku
zinapita, lakini Simba wanaendelea kuhangaikia ‘ Kiu Yao’ ya kurudi
miongoni mwa klabu mbili bora za Bara na hata kushinda ubingwa wa kwanza
tangu walipofanya hivyo mara ya mwisho msimu wa 2011/12. Simba
wanashindwa kuiangamiza kiu, lakini Kiu hiyo imekuwa ikiwaangamiza kwa
miaka mitatu mfululizo. Je, wataishinda Kiu hiyo msimu ujao?
USAJILI……
Achana
na usajili ulio mbioni kukamilika wa wachezaji Mreno, Ricardo de
Andrade ambaye ni mchezaji wa nafasi ya u-golikipa,Mshambulizi Mmali,
Makan Dembele, Straika Mrundi, Kevin Ndayisenga ambao wataungana na
Waganda, mlinzi wa kati, Juuko Murishid, kiungo, Simon Sserunkuma na
mshambulizi Hamis Kizza na Mzimbabwe, Justice Majabvi ambaye ana uwezo
wa kucheza nafasi ya ulinzi na ile ya kiungo.
Nyota
hawa saba wa kimataifa wanatazamwa kwa jicho la ‘ ukombozi’
wakichanganyika na sehemu ya timu iliyoandaliwa takribani miaka mitatu
iliyopita. Katika misimu mitatu ya mwisho kuelekea msimu wa 2015/16,
Simba imefanya usajili wa wachezaji wengi wa Kimataifa lakini tuseme
ukweli ni Emmanuel Okwi pekee ambaye amejitahidi kuisaidia klabu hiyo,
pia mchango binafsi wa mshambulizi Mrundi, Amis Tambwe msimu wa 2013/14
utaendelea kukumbukwa.
Okwi
alikuwa na matatizo ya nje ya uwanja-Kuchelewa kurejea klabuni kila
alipopewa ruhusa ya kwenda kwao lakini aliporejea na kupewa nafasi ya
kucheza alikuwa bora kuliko. Kama usajili huu Utalipa kwa Simba wanaweza
kufanya vizuri na kukata kitu yao licha ya kwamba hawataimaliza. Nyota
wa kimataifa wamekuwa na mchango mkubwa kwa klabu za Azam FC na Yanga SC
katika kipindi cha misimu mitatu iliyopita lakini kwa Simba wamekosa
utulivu na wengi licha ya kusajiliwa kwa matarajio makubwa hushindwa na
kuondoolewa mapema.
NYOTA WAPYA WENYE UZOEFU……
Mashabiki
wa Yanga SC wanasema Musa Hassan Mgosi ni ‘ Mzee’, lakini sivyo, kama
Musa atajibidiisha anaweza kuwa mfungaji bora wa muda woote wag emu za ‘
Dar es Salaam derby’. Mgosi amekwisha funga mara nne katika mipambano
ya Simba na Yanga na msimu wa mwisho alifunga mara mbili katika ushindi
wa Simba 4-2 Yanga, April, 2011. Simba wenyewe hawana shaka kuhusu Musa
kwa kuwa hivi sasa ni mchezaji anayepevuka zaidi kiakili, kiuchezaji na
nidhamu.
Kitendo
cha kupewa u-nahodha wa klabu hiyo kwa mara nyingine kitachochoea uwezo
wake na ataendelea kufunga mabao muhimu hata kama hatooshinda tena tuzo
ya ufungaji bora kama alivyofanya misimu mitano iliyopita. Mgosi
anaungana na kijana Daniel Lyanga kama maingizoo mapya ‘ wazawa’ katika
safu ya mashambulizi. Bila shaka wataziba nyufa hizo vizuri sambamba na
washambuaji wapya waliosajiliwa kutoka ng’ambo ya nchi.
Peter
Mwalyanzi ni mchezaji wa nafasi ya kiungo wa mashambulizi, huyu ana
uwezo wa kucheza kama wing pia. Ni mchezaji mwenye kasi na mzuri katika
kumiliki mpira, alicheza vizuri kiasi katika pambano dhidi ya SC Villa
ya Uganda siku ya Jumamosi iliyopita na alionesha kuwa Simba haikukosea
kumsaini kutoka Mbeya City FC. Mlinzi wa kati, Mohamed Fakhi na Yule wa
pembeni Samih Hajji Nuhu pia wameongezwa kuongeza namba ya walinzi.
Usajili
huu unaweza kutosheleza kiu ya klabu, mashabiki na wapenzi?. Chini ya
mwalimu raia wa Uingereza, Dylan Kerry na wasaidizi wake, Suleimani
Matola ( koocha msaidizi), Idd Salim ( kocha wa magolikipa) na mtaalamu
wa mazoezi ya viungo, Mromania, Momeilovic Dusan timu hiyo
haitashindwa kirahisi msimu ujao kwa kuwa utawala umeonekana kuwa makini
katika usajili na uboreshaji wa benchi la ufundi. Nyota wapya na timu
mpya ya ufundi wanaweza kushilikiana vizuri na nyota waliowakutana na
kutengeneza ‘ sura ya matumaini’.
Simba
haijakosea kumsaini kwa mara ya pili kiungo Mwinyi Kazimoto kwa kuwa
timu ilihitaji wachezaji wazoefu wenye uwezo kama Mwinyi, Mgosi, Kizza
na wengineo. Nafikiri Ingizo la Lyanga litageuka kutoka usajili wa
kawaida hadi kuwa mchezaji muhimu. Kwa usajili Simba hawajakosea sana
wamejitahidi kwa kiasi cha kuridhisha.
WACHEZAJI VIJANA……..
MANYIKA
Peter Jr, Hassan Kessy, Mohamed Hussein ‘ Tshabalala’, nahodha msaidizi
Hassan Isihaka, Juuko, Abdi Banda, Said Ndemla, Jonas Mkude, Simon,
Ibrahim Ajib ni baadhi ya wachezaji vijana watakao endelea kuichezea
klabu hiyo msimu ujao. Simba ilisemwa kutokuwa na uzoefu wa wachezaji
hao katika ligi kuu ndiyo kumesababisha washindwe kufanya vyema katika
ligi kuu na wao walichukulia kama sababu ya kuficha udhaifu wa timu
ndani ya uwanja.
Je,
nyota hawa vijana ambao wanakwenda kucheza msimu wan ne katika ligi kuu
watakuwa wamejifunza na kujiongezea mbinu na maarifa zaidi ili
kuisaidia klabu yao msimu ujao?. Ibrahim Twaha, Abdallah Seseme,
Ramadhani Singano, Okwi, Elius Maguli, Hussein Sharrif, William Lucian
ni baadhi ya vijana ambao wameondooka klabuni msimu huu ili kupisha
wachezaji wapya wenye uzoefu.
Kundi
la vijana kina Isihaka ni lazima sasa wawe na kiu ya kushinda ubingwa
wa Tanzania Bara kwa kuwa kutofanya hivyo msimu ujao klabu itakuwa
imekaa kwa miaka minne mfululizo pasipo kushinda ubingwa huo. Simba
iliwahi kusubiri kwa miaka minne kushinda ubingwa wa kwanza wa ligi kuu.
Kati ya 1996 hadi mwaka 2000 timu hiyo ya ‘ Mtaa wa Msimbazi’ iliishi
bila kushinda ubingwa wa ligi.
Sasa
hakuna tena kisingio cha ukosefu wa uzoefu, Simba watapaswa tu kupiga
na kushinda moja ya nafasi mbili za juu na wachezaji vijana wanatakiwa
kusahau kuhusu umri wao na kucheza kwa malengo ya kushinda tu.
HOFU…….
Baada
ya kuwaajiri walimu wa kutosha katika benchi la ufundi, labda sasa
utawala unapaswa kujirekebisha na tatizo lao la mar azote-Kuingilia na
kushinikiza maamuzi yao kwa benchi la ufundi. Makocha wooote wa klabu
hiyo wamekuwa wakilalamikia hali hiyooo mara baada ya kufukuzwa lakini
afadhali kwa Mserbia, Goran Kopunovic ambaye alionekana kuwa huru katika
kazi yake.
Simba
itafanikiwa kumaliza kiu mojawapo ( kumaliza nafasi ya pili au kushinda
ubingwa) ikiwa tu wachezaji watajituma, watacheza kwa usikivu na
kufuata maelekezo ya benchi la ufundi. Kiu ya mafanikio imewaganda
mashabiki na wapenzi wa klabi hiyo. Kiu hii itamalizwa kama kila mtu
atafanya kazi yake kwa uhuru, vinginevyo Azam FC na Yanga SC zitaendelea
kutawala nafasi mbili za juu
0 comments:
Post a Comment