STRAIKA wa KRC Genk ya Ubelgiji na
nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Mbwana Samatta
amekuwa nyota wa Tanzania ambaye amejizolea tuzo nyingi tangu aanze
kufahamika. Mtandao wa BOIPLUS
uliamua kumtembelea nyumbani kwake ili kujua anazihifadhi vipi tuzo na
medali zote alizowahi kutunukiwa. Hizi hapa ni baadhi ya picha:
Ukifika tu nyumbani kwake utakaribishwa
na kabati kubwa lililopambwa kwa medali, vyeti na tuzo mbalimbali
alizowahi kutwaa mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba Sc na TP Mazembe
ya DR Congo
Licha ya kutisha awapo uwanjani, kumbe
Samatta ni mtaalamu wa matumizi ya kiofisi ya kompyuta. Hiki hapa ni
cheti chake alichotunukiwa baada ya kuhitimu mafunzo hayo
Mara kadhaa Chama cha Waandishi wa
Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kimekuwa kikimpatia tuzo Samatta kwa
kuthamini mchango wake kwenye Tasnia ya michezo nchini, hiki hapa ni
cheti alichotunukiwa na TASWA 2015
Katika msimu wa 2013/14, TASWA ilimtaja
Samatta kama Mchezaji Bora anayecheza nje ya nchi. Na hii hapa ndio
tuzo yake ambayo inapamba kabati lake pia
Mwishoni mwa mwaka jana, Samatta akiwa
na TP Mazembe alishiriki michuano ya Kombe la Dunia kwa ngazi ya Klabu
huko Japan. Mazembe haikufanya vizuri lakini wachezaji walipewa tuzo za
ushiriki ambayo inaonekana hapo juu
TASWA pia ilimpatia tuzo ya Mchezaji mwenye Mafanikio ndani ya miaka 10 kuanzia 2005 hadi 2015
Tuzo nyingine ambayo inapatikana ndani ya kabati la Samatta alipewa na mtandao wa GOAL.COM kama mchezaji bora wa mwaka 2014
2011 akiwa anaitumikia klabu ya Simba
SC ya jijini Dar es Salaam alishiriki michuano ya Mapinduzi Cup na
kufanikiwa kupata medali ya dhahabu.....nayo ilikutwa imehifadhiwa
mahali pake ndani ya kabati
Mwaka jana ulikuwa wa mafanikio makubwa
kwa Samatta, licha ya kuvaa medali ya dhahabu ya michuano ya Klabu
Bingwa barani Afrika, mkali huyo wa mabao aliyeanzia soka lake katika
viunga vya Mbagala jijini Dar, alifanikiwa pia kuwa mfungaji bora wa
michuano hiyo
Hii ndio tuzo kubwa kabisa ya binafsi
aliyowahi kutwaa Samatta, alitangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Afrika kwa
wanaocheza ligi za ndani
Na hiki ni cheti kilichoambatana na tuzo hiyo ya Afrika
2010 Samatta aliungana na vijana
wenzake wa Timu ya Taifa ya vijana (U20) huko nchini Eritrea na
wakafanikiwa kutwaa medali ya dhahabu katika michuano iliyoandaliwa na
CECAFA
Gazeti la michezo la Mwanaspoti
lilimtaja Samatta kuwa Mchezaji Bora wa Tanzania anayecheza nje ya nchi.
Hiyo ilikuwa katika msimu wa 2012/13
Wengi walimfahamu Samatta akiwa African
Lyon ambako alifanya mambo makubwa hadi kuwatamanisha Wekundu wa
Msimbazi Simba. Msimu wake wa mwisho akiwa Lyon, Samatta alionyesha
uwezo mkubwa ikiwemo kufunga mabao mengi hadi klabu hiyo ikaamua
kumtunukia Medali hii maalum
Kwa uzalendo alionao kwa taifa lake,
ndani ya kabati hilo Samatta ameweka 'Scarf' ya bendera ya Taifa huku
akieleza kuwa anajivunia sana kuwa Mtanzania
Akiwa TP Mazembe, Samatta alifanikiwa
kufunga 'Hattrick' tatu, na hii hapa ndio mipira aliyoondoka nayo huko
DR Congo. Hata hivyo straika huyo anasikitika kupotelewa na mpira mmoja
ambao alikabidhiwa baada ya kupiga Hattrick akiwa Simba SC
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment