MAWASILIANO

Phone. - +255 (717) 300 260 - +255 (787) 300 260

HABARI YA MUJINI

HABARI YA MUJINI
watu wa mpira

HII NDIYO MO BEJAIA ITAKAYOKUTANA NA YANGA KWENYE MCHEZO WA KWANZA HATUA YA MAKUNDI




Bejaia
Na Johnson Kashushura
Kuelekea kinyang’anyiro cha kuwania kombe la Shirikisho barani Afrika, ambapo mabingwa wa Soka Tanzania Bara Yanga wamo pia, tunakuletea mfululizo wa wasifu wa vilabu ambavyo Yanga itakwaana navyo katika hatua ya makundi.
Mfufulizo wa kuzichambua timu ambazo zitakutana na Yanga hautaishia tu kwenye makundi bali kadri Yanga itakavyozidi kusonga mbele na sisi ndivyo tutakavyozidi kuzitupia macho.
Kama ilivyotangazwa hapo jana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), michezo ya hatua ya makundi itaanza kuchezwa June 17 mwaka huu ambapo Yanga itaanzia ugenini dhidi ya MO Bejaia ya Algeria.
Katika hali yoyote ile inahitajika umakini mkubwa kwa Yanga ili kuweza kufanya vizuri katika hatua hii na kwenda hatua ya nusu fainali.
Si jambo rahisi lakini muhimu ni kuhakikisha Yanga ama anapata sare ugenini au kushinda na kuhakikisha kuwa anashinda mechi zake za nyumbani ili kuweza kujitengenezea mazingira mazuri ya kufuzu mapema bila kikwazo.
Yanga ipo kundi A pamoja na timu za TP Mazembe ya DRC, MO Bejaia ya Algeria na Medeama ya Ghana.
Leo tunawaangazia waarabu wa Algeria, MO Bejaia, ungana nami kujua zaidi kuhusu klabu hii ambayo itacheza dhidi ya Yanga mchezo wa kwanza hatua makundi ya kombe la shirikisho.
MO Bejaia ni kifupi cha neno Mouloudia Olympique de Béjaïa. Hawa pia wanafahamika kwa kifupisho cha jina la MOB.
Hii ni timu inayotokea katika jiji la Béjaïa, lililopo Kaskazini mwa Algeria. Inashiriki ligi kuu nchini humo maarufu kama Algerian Ligue Professionnelle 1, ilianzishwa mwaka 1954.
Mo Bejaia inatumia uwanja wake wa nyumbani unaojulikana kwa jina la  l’Unité Maghrébine (Stade de l’Unité Maghrébine).
May 2015, MO Béjaïa ilijinyakulia kombe la Algeria maarufu kama Algerian Cup. Iliichukua ndoo hiyo baada ya kuichapa RC Arbaâ 1-0. Kombe hili ndilo lilowapa nafasi ya kushiriki michuano hii ya kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation).
Historia ya vikombe tangu ianzishwe.
Mo Bejaia wamechukua makombe mawili tu kuanzishwa kwao, makombe hayo ni Ligue Nationale msimu wa 2010–11 na kombe la Algerian Cup mwaka 2015.
Kwa sasa kikosi chao kinaundwa na wachezaji 26 ambapo kati yao wageni ni watatu tu.
Kwa sasa MO Bejaia wanashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Algeria wakiwa na pointi 43 wakiwa nyuma kwa pointi 15 dhidi ya vinara USM Alger wenye pointi 58.
Mchezo wa ligi waliocheza Ijumaa ya May 20 waliwafunga MC Alger kwa mabao 2-0, mchezo uliopigwa katika dimba lao la nyumbani la Stade de l’Unité Maghrébine.
Hawa ndio wachezaji wanaounda kikosi cha MO Bejaia

 Hili ni benchi lao la ufundi
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment