MAWASILIANO

Phone. - +255 (717) 300 260 - +255 (787) 300 260

HABARI YA MUJINI

HABARI YA MUJINI
watu wa mpira

SIO TU KAZI YA USEMAJI, HATA HUMU MANARA PIA YUMO


Afisa habari wa Simba SC Hajji Manara (kulia) akikabiliana na mchezaji wa wacheza filamu wa Bongo Movies
Afisa habari wa klabu ya Simba Hajji Manara jana alikuwa kivutio kikubwa kwenye siku ya Simba Day pale alipoingia uwanja kuonesha kipaji chake cha soka wakati timu yake ya viongozi wa Simba SC ilipokuwa ikicheza na wacheza filamu wa Tanzania (Bongo Movies) mchezo uliokuwa wa utangulizi kabla ya mechi ya Simba SC haijacheza na Sports Club Villa ya Uganda.
Simba day 8Manara aliingia uwanjani akitokea benchi na mara baada ya kuanza kucheza mpira mashabiki wa timu hiyo walianza kumshangilia Manara ambaye amekuwa na maneno mengi tangu alipopewa wadhifa wa kuwa afisa habari wa klabu hiyo.
Simba day 19Hata hivyo Manara hakucheza dakika zote zilizokuwa zimesalia kwani alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na kiongozi mwingine wa klabu hiyo.
Simba day 8Manara alisema mbali na kuwa msemaji wa Simba, yeye anakipaji cha kucheza mpira na amekuwa akicheza mpira tangu shule ya msingi.
Simba day 4Viongozi wa klabu ya Simba walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 mbele ya waigizaji wa Bongo movies goli lililowekwa kambani na kocha mkuu wa Simba SC Dylan Kerr.
Simba day 18


09 Aug 2015

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment