MAWASILIANO

Phone. - +255 (717) 300 260 - +255 (787) 300 260

HABARI YA MUJINI

HABARI YA MUJINI
watu wa mpira

IVO MAPUNDA ‘ SHUJAA’ ANAYEONDOLEWA NA ‘ CHUKI’ SIMBA SC


Na Ben Shija, Dar es Salaam
Baada ya miaka miwili na nusu kuichezea Simba SC hatimaye golikipa Ivo Mapunda ataondoka katika klabu hiyo baada ya kumalizika kwa mkataba wake. 
Ivo, golikipa wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars na klabu za Tukuyu Stars, Tanzania Prisons, Moro United, Yanga SC, St.George ya Ethiopia, African Lyon alijiunga na Simba, Desemba, 2013 akitokea Gor Mahia FC ya Kenya alifanya mazungumzo ya kusaini mkataba mpya kabla/baada ya kumalizika kwa ligi kuu msimu uliopita lakini Jumatatu hii klabu.
Ivo alisajiliwa Simba ili kusahihisha makosa ya mlinda mlango, Mganda, Abel Dhaira ambaye kwa mtazamo wangu ndiye kipa ' dhaifu' zaidi kuwahi kuichezea timu hiyo katika kipindi cha miaka 15 sasa. 
Dhaira alisainiwa kama mbadala wa aliyekuwa kipa namba moja wa muda mrefu, Juma Kaseja wakati wa usajili wa dirisha dogo, Desemba, 2012.
Mganda huyo alikuwa akitoka hovyo golini huku akitema mipira mara kwa mara, nakumbuka alifungwa mabao ya kizembe katika sare ya Simba 2-2 na Mbeya City, Septemba, 2013 wakati alipofungwa goli la mbali na Paul Nonga. 
Pia, Dhaira ndiye mchezaji aliyedaka katika sare ya Yanga 3-3 na Simba, Oktoba, 2013 na baada ya mechi hiyo mashabiki wakahitaji mabadiliko ambayo yalishuhudia IVO akitua katika timu hiyo huku akiwa mshindi wa ligi kuu ya Kenya.
Akiwa ametoka kufanya vyema katika michuano ya Cecafa Challenge Cup nchini Kenya, Ivo alikataa kusaini mkataba mpya na Gor na kuamua kurejea nyumbani na kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2007 akashiriki katika pambano la mahasimu wa soka nchini, Yanga na Simba katika mchezo wa Hisani wa Nani Mtani Jembe-1, 2013. S
imba ilishinda 2-0 huku IVO akicheza kwa kiwango cha juu. Dhaira akaondoka zake na mara baada ya kumalizika kwa msimu wa 2012/13 baada kuwa msugua benchi. 
Mtibwa Sugar 1-1 Simba SC, Mgambo JKT 2-1 Simba SC, Simba SC 1-2 Kagera  Sugar…. 
Mechi hizi Tatu hakika Ivo hatazisahau. Akiwa ameanza vizuri katika Mtani Jembe, kipa huyo aliendeleza kiwango cha juu hadi alipokuja kuruhusu bao la umbali mrefu wakati timu yake ilipocheza na Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro katika mchezo wa ligi kuu, Februari, 2014. Musa Hassan Mgosi alipiga mpira mrefu ‘ kama krosi’ ambayo ilisogwa na upepo na kuelekea golini kwa kasi. Mpira huo ulimshinda Mapunda na kutinga nyavuni.
Siku chache baadaye Mapunda alilaumiwa wazi na mashabiki wa klabu ya Simba baada ya kufungwa goli rahisi katika mchezo ambao Simba ililazwa 2-1 na Mgambo JKT katika uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Hizo zilikuwa mechi mbili ambazo, Ivo zilianza ‘ kumuweka njia panda’. Ilikuwa ni katika michezo ya mzunguko wa pili msimu wa 2013/14.
Msimu wa 2014/15 Simba ilikuwa na magolikipa watatu, Ivo Hussein Shariff ambaye alisajiliwa akitokea Mtibwa huku mkono akiwa na tuzo ya kipa bora wa ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2013/14, pia alisajiliwa kijana wa timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania, Manyika Peter Manyika ‘ Manyika Jr’.
Ivo ambaye tayari alikuwa amecheza gemu mbili mfululizo ya ‘ Dar es Salaam derby’ na  kuruhusu nyavu zake mara  moja akaendelea kuwa kipa chaguo la kwanza cha Mzambia, Patrick Phiri hadi pale aliporuhusu magoli mawili ya ‘ kizembe’ katika kipigo cha Simba 1-2 Kagera Desemba, 2014 katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Alidaka vizuri katika mchezowa Mtani Jembe-2. Gemu ambayo Simba iliishinda Yanga 2-0.
Baada ya kutishia kuachana na klabu hiyo mara baada ya kusakamwa sana kufuatia kuruhusu magoli rahisi aliyekuwa mwalimu wa  timu hiyo, Phiri aliwajibu baadhi ya viongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa hawapaswi kumlaumu Ivo bali wamlaumu yeye ambaye alimpatia amliptatia nafasi ya kucheza.
Manyika akapangwa kwa mara ya kwanza katika mchezo wa Simba 0-0 Yanga, oktoba , 2013 baada ya Ivokuwa na majeraha ya kidole huku Shariff akiwa na majeraha makubwa ya mguu. Kijana huyo ambaye alikuwa akiichezea Simba kwa mara ya kwanza aliweza kufanya vizuri kiasi cha kutajwa kama mrithi wa kweli ya Kaseja, lakini baada ya muda mfupi Manyika akapoteza nidhamu kiasi cha kudili zaidi na watu waliokuwa wakimkosoa na kuachana kuwekeza mkazo katika kurekebisha makosa yake ya kutoka hovyo langoni. 
Ivo alipona na kuanza kushindania namba na Manyika na kushinda vita hiyo. Atakumbukwa kwa mipambano minne aliyocheza dhidi ya Yanga kwani alikuwa kama ‘ hirizi ya bahati’ ya klabu ya Simba kwani katika gemu Tano za mwisho za mahasimu hao wa soka nchini zimeshuhudia Yanga ikifunga mara moja tu. Mechi ya mwisho kwa Ivo ambayo pia ilikuwa ni ya nne kwake ilikwisha kwa Simba kushinda 1-0 Machi mwaka huu katika VPL.
Ivo anaondoka Simba akiwa shujaa anayechukiwa kisirisiri kwani ameshinda mataji mawili ya Mtani Jembe, Moja la Mapinduzi Cup huku akiwa ameshinda mechi tatu kati ya Nne alizocheza dhidi ya Yanga SC. Mechi Tatu alizobonga kwangu haziwezi kufuta sifa yake nzuri ya uaminifu kwa klabu ya Simba, alichezea kwa moyo na kama mchezaji wakati mwingine alifanya makosa. Ivo si Shujaa wa Simba Pekee, ameshinda VPL 2 akiwa Yanga, Ubingwa wa ligi kuu ya Ethiopia na Kenya alikuwa shujaa kwa mashabiki wanazi wa Gor….
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment