BOBAN, IDDI MOSHI 'MNYAMWEZI' WAPATA MSIBA WA BABA YAO
Mzee Moshi Shabani
amefariki dunia leo jijini Dar es Salaam.
Moshi ndiye baba wa
wanasoka maarufu nchini ambao ni Mrisho Moshir, Iddi Moshi ‘Mnyamwezi’, Ally
Moshi na Haruna Moshi ‘Boban’.
Akizungumza na BEN SHIJA,Boban alisema mzee wake amefariki baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa mapafu.
"Mzee
katutoka, Mwenyezi Mungu amemuhitaji leo saa sita na nusu mchana.
Tunatarajia mazishi yatakuwa kesho mchana, inshallah" alisema.
Marehemu ambaye alikuwa
mwajiriwa wa muda mrefu wa Shirika la Reli Tanzania, amefariki baada ya kuugua
muda mrefu.
Taratibu za mazishi zinaendelea na tutawataarifu.
0 comments:
Post a Comment