Jana tarehe 2 – 9 – 2015 Uongozi wa Simba ukiongozwa na Rais wa Simba Evans Aveva ulikutana na viongozi wa matawi ya Dar es Salaam pamoja na mikoa ya Karibu katika kikao kilichofanyika ofisi za makao makuu ya klabu ya Simba jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano huo ulioanza majira ya saa 8 kamili mchana na kumalizika saa 12 kamili jioni Rais wa Simba Evans Aveva alipata nafasi ya kuongea na kuwasikiliza viongozi wa Simba katika dhima ya kujenga klabu ya Simba. Rasi wa Simba Evans Aveva katika mkutano huo alisema “umoja ni nguvu, na bila umoja hakuna kitu kinachoweza kufanyika ni mambo mengi Simba imeyapanga na mazuri lakini umoja siku zote wanasimba ndio nguzo ya Mafanikio na hivyo hatuna budi viongozi na wanachama kudumisha umoja”.
Rasi Evans Aveva pia alipata nafasi ya kuongelea maandalizi ya klabu ya Simba kwa msimu mpya wa ligi na kusema “maandalizi yanakwenda vizuri sana na mpaka sasa tumesha sajili wachezaji 27 katika kikosi chetu cha Simba tayari kuanza kwa ligi, ni imani yangu kubwa sana kwamba tutakipa ushirikiano kikosi hicho cha Simba pamoja na benchi lote la ufundi na hivyo kuleta ushindi kwa wanasimba”
Akizungumza kwenye mkutano huo mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba na makamu mwenyekiti wa kamati ya matawi na wanachama Iddi Kajuna alisema ” Simba inatoa kipaumbele kwa wanachama wake na inatambua umuhimu wa viongozi wa matawi katika kujenga umoja na mafanikio kwa klabu ya Simba”.
Katika mkutano huo pia alialikwa Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya EAGgroup Limited Imani Kajula ambao ni washauri na watekelezaji wa masuala ya kibiashara na masoko wa klabu ya Simba ambapo alipata nafasi ya kuwafafanulia kwa undani mipango ya Simba kibiashara zaidi. “mafanikio ya kibiashara na kuifanya chapa ya Simba kuwa moja Kati ya chapa bora ni Lengo kuu ambalo EAG Group imekabidhiwa, Tayari tumeanza kufanya kazi na tutaendelea kuwa Karibu na viongozi wa matawi katika kuleta maendeleo ya kimasoko na biashara kwa klabu ya Simba” Alisema Imani Kajula.
Simbasports.co.tz inawatakia maandalizi mema wanachama na viongozi wote wa Simba katika kuanza kwa ligi kuu ya Tanzania Bara 2015/2016 pamoja na mafanikio katika mipango yote ya kuendeleza klabu ya Simba.
0 comments:
Post a Comment