MAWASILIANO

Phone. - +255 (717) 300 260 - +255 (787) 300 260

HABARI YA MUJINI

HABARI YA MUJINI
watu wa mpira

SDF WAFANYA UCHAGUZI

TAWI la Simba Damu Fans (SDF) leo limefanya uchaguzi wake mkuu ambao umewaweka madarakani viongozi wapya kwa mujibu wa Katiba yao, uchaguzi huo umefanyika Makao Makuu ya tawi hilo lililopo Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam


Karim Boimanda ambaye alitetea nafasi yake amechanguliwa kuongoza tawi hilo tangu kuanzishwa kwa tawi hilo kwa miaka minne ijayo kwa kupata kura 20 kati ya 30 zilizopigwa huku Severin Machila akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti kwa kupata kura 23 na kumbwaga mpinzani wake Rakhim Rashid aliyepata kura nne.

Wajumbe wa kamati ya Utendaji waliochaguliwa ni Mohamed  Nammenge, Rashid Ntimizi na Alfej Kehongo.

Wajumbe walioteuliwa na Kamati ya Utendaji ni Ally Masaninga (Katibu Mkuu), Mathew Kawogo (Afisa Mipango na Uchumi), Ally Shatry 'Chico' (Afisa Habari na Mahusiano) pamoja na Bernard Chezue (Mhasibu)

Mwenyekiti wa SDF pia amewateuwa wajumbe wawili (kwa mujibu wa Katiba) kuingia kwenye Kamati ya utendaji ambao ni Hamza Mahosanya na Devotha Isisha.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment