Mama mzazi wa Mwenyekiti wa Usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe amefariki dunia leo jijini Dar es Salaam.
Anna Mercati ,84, amefariki dunia na msiba wake uko Ununio nyumbani kwa mwanaye Hans Poppe.
Akizungumza na BEN SHIJA, Hans Poppe amesema mwili wa mama yake utaagwa saa 4 asubuhi siku ya Jumamosi na baada ya hapo safari ya kwenda Iringa kwa mazishi itaanza.
“Baada ya kuagwa, tutaanza safari ya kwenda Iringa na inshallah, Jumapili ndiyo mazishi,” alisema Hans Poppe.
Hivyo Jumamosi itakuwa nafasi kwa rafiki, ndugu, jamaa na wadau wa soka kutoka klabu, vyama na mashirikisho mbalimbali kumuaga mama wa mdau huyo maarufu wa soka nchini.
0 comments:
Post a Comment