Na Ben Shija, DAR ES SALAAM
KIPA chipukizi, Peter Manyika jana ameidakia Simba SC kwa mara ya 25 tangu ajiunge nayo msimu uliopita na akafungwa bao la 20.
Simba SC jana imeshinda mabao 2-1 dhidi ya URA ya Uganda Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na mtoto wa kipa wa zamani wa kimataifa nchini, Manyika Peter alikuwa langoni.
Pamoja na kufungwa bao moja, Manyika alidaka vizuri na kuzidi kujijengea nafasi mbele ya kocha Muingereza Dylan Kerr, Simba SC ikiibuka na ushindi wa 2-1.
Manyika alisajiliwa msimu uliopita Simba SC kama kipa wa timu ya vijana chini ua umri wa miaka 20 na kipa wa tatu wa kikosi cha kwanza, lakini kuumia mfululizo kwa makipa wa juu yake, Ivo Mapunda na Hussein Sharrif ‘Casillas’ kukampa nafasi mapema kikosi cha kwanza.
Baada ya msimu, Simba SC imemuacha Casillas wakati hadi sasa haijamuongezea Mkataba mpya Mapunda huku ikiwa mbioni kusajili kipa mpya, Vincent Angban kutoka Ivory Coast.
Manyika anaingia katika mwaka wake wa pili na wa mwisho wa Mkataba wake Msimbazi- timu ikiwa chini ya kocha mpya, Kerr- maana yake anahitaji kujibidiisha ili kupigania Mkataba mpya.
Peter Manyika jana alidaka dakika zote 90 na kufungwa bao Simba SC ikishinda 2-1
Peter Manyika jana alidaka dakika zote 90 na kufungwa bao Simba SC ikishinda 2-1
REKODI YA PETER MANYIKA SIMBA SC
Simba SC 0-0 Orlando Pirates (kirafiki aliingia dk43 hakufungwa, Afrika Kusini)
Simba SC 2-4 Bidvest Witss (Kirafiki, alifungwa nne Afrika Kusini)
Simba SC 2-4 Bidvest Witss (Kirafiki, alifungwa nne Afrika Kusini)
Simba SC 0-2 Jomo Cossmos (Kirafiki, alifungwa mbili Afrika Kusini)
Simba SC 0-0 Yanga SC (Ligi Kuu, hakufungwa)
Simba SC 1-1 Prisons (Ligi Kuu, alifungwa moja)
Simba SC 1-1 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu, aliokoa penalty, akafungwa moja)
Simba SC 0-0 Express (Kirafiki, hakufungwa)
Simba SC 0-1 Mtibwa Sugar (Kombe la Mapinduzi, Zanzibar alifungwa moja)
Simba SC 1-0 Mafunzo (Kombe la Mapinduzi, Zanzibar hakufungwa)
Simba SC 1-0 JKU (Kombe la Mapinduzi, hakufungwa)
Simba SC 4-0 Taifa Jang’ombe (Robo Fainali Kombe la Mapinduzi, hakufungwa)
Simba SC 1-0 Polisi (Nusu Fainali Kombe la Mapinduzi, hakufungwa)
Simba SC 0-0 Mtibwa Sugar (Alimpisha Ivo dakika ya 90, Simba ikashinda penalti 4-3 Fainali Kombe la Mapinduzi)
Simba SC 2-0 Ndanda FC (Ligi Kuu Mtwara, hakufungwa)
Simba SC 1-1 Azam FC (Ligi Kuu, alifungwa moja)
Simba SC 1-2 Mbeya City (Ligi Kuu Taifa, alifungwa mbili)
Simba SC 2-0 Polisi Moro (Ligi Kuu, aliingia kipindi cha kwanza kumalizia baada ya Ivo kuumia, hakufungwa)
Simba SC 0-2 Mgambo Shooting (Ligi Kuu, alifungwa moja baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Ivo aliyetolewa kwa kadi nyekundu kipindi cha pili)
Simba SC 3-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu, hakufungwa)
Simba SC 2-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu, alifungwa moja)
Simba SC 3-0 Toto Africans (Kirafiki Mwanza, aliingia kipindi cha pili hakufungwa)
Simba SC 2-0 Mbeya City (Alifungwa mbili, Ligi Kuu)
Simba SC 2-1 Zanzibar Kombaini (Alifungwa moja, Kirafiki Zanzibar)
Simba SC 4-0 Black Sailor (Hakufungwa Kirafiki Zanzibar)
Simba SC 3-2 KMKM (Alifungwa mbili, akatolewa kipindi cha pili, Kirafiki Zanzibar)
0 comments:
Post a Comment