Kikosi cha Simba imeendeleza kufanya ubabe katika mechi zake za kirafiki visiwani hapa, baada ya juzi kushinda mchezo wake wa tatu mfululizo ilipoizabua timu ya Polisi inayoshiriki Ligi Kuu Zanzibar kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Amaan.
Matokeo hayo yamempagawisha kocha msaidizi wa timu hiyo, Suleiman Matola ambaye amesema kiwango cha wachezaji wake kimepanda na wanachosubiri ni kufanya maangalizi tu kwenye ligi kuu.
Awali, Simba iliichapa Kombaini ya Zanzibar na baadaye ikainyuka Black Sailors.
Katika mchezo wa juzi, mkongwe Mussa Hassan Mgosi aliwainua mashabiki a Simba dakika ya pili kwa bao safi akiunganisha krosi ya kushoto ya beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’. Mshambuliaji mwenye nguvu aliyetamba atavaa viatu vya Okwi, Elius Maguli alipiga bao jingine baada ya kuitendea haki kazi nzuri iliyofanywa na beki Kessy Ramadhan.
“Ujio wa Mwinyi Kazimoto nao umetuletea hamasa kubwa, kwa hiyo kikosi kipo vizuri na tunatarajia kufanya mambo makubwa ligi itakapoanza,” alisema Matola baada ya mchezo huo.
0 comments:
Post a Comment