Baada ya Mradi wa Mabasi ya Mwendokasi, Treni, Kivuko cha Mv. Dar es Salaam, leo kuna taarifa nyingine nzuri ambayo inahusu jitihada za Serikali kumaliza tatizo sugu la foleni katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Taarifa iliyoripotiwa na kituo cha TBC1, Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli amesema; “… Tuliwatuma wataalamu hawa, na bahati nzuri Chief Executive wa TANROADs hivi karibuni na wataalamu wenzake walienda South Korea.. Serikali ya South Korea imekubali kutufadhili kujenga flyover nyingine pale.. na barabara yenyewe itakuwa na urefu wa karibu kilomita 7.2 na barabara itaanzia Coco Beach, itapita baharini itakuja kutokea Agakhan Hospital na kuja ku-join na barabara nyingine hii ya Alli Hassan Mwinyi…”
“.. Tumepanua maeneo pengine kote.. tuna mradi wa BRT ambao una-involve kilometa zaidi ya ishirini na moja na karibu sasa hivi unaisha chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia, lakini tunapofika pale Salenda pamekuwa na tatizo kubwa na kwa sasa hivi katika traffic count ya magari yanayopita pale kwa siku yamezidi zaidi ya magari hamsini na moja elfu kwa hiyo hawawezi wakaya-accommodate magari yote yanayoweza kupita sehemu hiyo…”– Dk. Magufuli
About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment