Real M adrid iko mbioni kutimiza mwaka wake wa 10 huku ikiwa inaongoza kama taasisi ya michezo linapokuja suala la mapato au faida inayotengenezwa.
Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na rais wa klabu hiyo Florentino Perez ambaye alikuwa akitangaza taarifa ya mapato na matumizi ya klabu hiyo kwa mwaka wa kibiashara ulionendana na msimu wa mwaka 2013/2014 mwezi septemba mwaka huu ..
Kama taarifa zinavyopaswa kuwa , taarifa hii ni sahihi kwa asilimia 100% lakini kiundani haina maana yoyote katika uhalisia wa mapato.
Kitu ambacho Perez alishindwa kukijumuisha katika taarifa hiyo ni ukweli kwamba klabu ya Real Madrid ilimaliza kipindi hicho hicho ikiwa na deni la euro milioni 602 , deni ambalo kwa kufananisha na la mwaka uliopita limeongezeka kwa euro milioni 61 .
Deni hili limetokana na mkopo wa euro milioni 283 huku madnei mengine yakiwa yanatimiza kiasi cha euro milioni 459 toka kiwango cha euro milioni 396 kwa kipindi cha miezi 12 .
Kwa kifupi mapato ambayo Madrid iliyapata hayajaweza kufanya deni hili lififie hali inayomaanisha kuwa kiukweli Madrid inapoteza fedha nyingi kuliko zile inazoingiza .
Madrid inadaiwa na zaidi ya mdeni mmoja , na taasisi kadhaa za kimichezo , klabu nyingine za soka , wachezaji na taasisi nyingine tofauti na michezo wote wanaidai klabu hii bingwa ya Ulaya .
Kwa hesabu nyepesi deni la Real Madrid kwa ujumla wake ni sawa na kuongeza kwa pamoja ada za uhamisho ambazo klabu hiyo ilitumia kuwasajili wachezaji wanne ambao ni Cristiano Ronaldo , James Rodriguez , Karim Benzema, Toni Kroos na Gareth Bale .
Kiasi cha fedha kilichotumiwa na PEREZ | Fedha zinazotumiwa kwa wachezaji kila mwaka |
Msimu | Fedha zilizoingia | Fedha zilizotoka | Tofauti |
2000-01 | €60.75m | €119.25m | -€58.5m |
2001-02 | €0 | €73.5m | -€73.5m |
2002-03 | €0 | €45m | -€45m |
2003-04 | €31.8m | €37.5m | -€5.7m |
2004-05 | €9.25m | €56.7m | -€47.45m |
2005-06 | €45.1m | €89.5m | -€44.4m |
2009-10 | €87.5m | €257.4m | -€169.9m |
2010-11 | €10m | €93m | -€83m |
2011-12 | €8m | €55m | -€47m |
2012-13 | €33.5m | €33.5m | €0 |
2013-14 | €114.5m | €166.5m | -€52m |
2014-15 | €114m | €122.5m | -€8.5m |
Jumla | €514.4m | €1.149bn | -€634.95m |
Chanzo: Mtandao wa transfermarkt
Kwa kifupi klabu ya Real Madrid haiwezi kuendelea kwa mtindo huu kwani kwa mujibu wa kanuni za usimamizi wa matumizi kwa vilabu vya soka barani ulaya yaani Financial Fair Play huenda Real Madrid ikakumbana na adhabu kama iliyotolewa kwa klabu za Paris St Germain na Manchester City hali inayoweza kushuhudia klabu hii ikizuiliwa kufanya usajili wa wachezaji wakubwa kama ilivyozoeleka kwenye desturi ya klabu hiyo .
About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment