Macho ya Watanzania Jumamosi Nov 29 2014 yalielekezwa kwenye utoaji wa tuzo za kituo kikubwa cha TV Afrika Channel O ambapo tuzo zilitolewa hapa Johannesburg South Africa huku Diamond Platnumz akiwa msanii pekee kutoka Tanzania kuchaguliwa kuwania tuzo hizi mwaka huu.
Furaha ya Watanzania ilikua kubwa baada ya kuona kijana kutoka nyumbani Tanzania Diamond Platnumz kushinda tuzo tatu kati ya nne alizokuwa anawania Most Gifted East,Most Gifted Afro Pop na Most Gifted Newcomer yaani msanii mpya.
Kwenye tuzo hizi Diamond aliambatana na mama yake mzazi pamoja na mrembo Zari wa Uganda ambae wamekua wakitajwa kwenye headlines sana na Diamond hivi karibuni.
Most Gifted R&B video
Crazy but Amazing-Donald
Most Gifted West Video
‘Turn Up-Olamide
Most Gifted Ragga/Dancehall
Buffalo Soulja
The Most Gifted Kwaito
Uhuru ft Oskido & Professor Kalawa -tjukutja
Most Gifted East Video
Diamond Platnumz
Most Gifted Dance Video
Busiswa-Ngoku
Most Gifted Hip Hop Video
AKA- Congratulate
Most Gifted Afro Pop Video
Diamond Platnumz
Most Gifted duo/group/featurning
KCEE ft Wizkid-Pull Over
Most Gifted Video of the Year
Carsper Nyovest- Dos Shebeleza
Most Gifted Newcomer
Diamond Platnumz
Most Gifted Male Video
Casper Nyovest-Doc Shebeleza
Most Gifted Female Video
Tiwa Savage-Eminado
Tuzo za 2014 za Channel O zimepata historia ya kipekee tofauti na siku nyingine ambazo Wanigeria ndio wamezoeleka kwamba wanashinda kwa wingi ila 2014 Diamond kutoka Tanzania na Carsper kutoka South Africa ndio wasanii pekee waliong’ara zaidi kwa kila mmoja kuondoka na tuzo zake tatu.
Kama Casper asingeshinda tuzo hiyo ya tatu basi Diamond ndio angekua amebeba tuzo nyingi zaidi kuliko msanii mwingine yeyote.
About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment