KIUNGO bora wa ulinzi wa Simba SC, Jonas Gerard Mkude amesema wachezaji wengi wa kitanzania wana malengo ya kucheza soka la kulipwa, lakini hawajitumi kutengeneza njia.
Mkude ambaye siku za hivi karibuni alisaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia Simba alisema kila mchezaji akiulizwa malengo yake anasema anataka kwenda ulaya, lakini jitihada za kwenda huko hazionekani.
“Unaweza kusema nina malengo ya kwenda ulaya, lakini ukawa unacheza hapa hapa tu kwasababu hujitumi. Kinachotakiwa kwa sisi wachezaji ni kujiongeza zaidi kimazoezi ili kuwa fiti kwa changamoto za kimataifa”. Alisema Mkude.
“Nina ndoto za kwenda kucheza soka la kulipwa, lakini inabidi nijitume hapa nilipo ili kusonga mbele”.
Mkude ambaye ni kipenzi kikubwa cha mashabiki wa Simba aliongeza kuwa kikosi chao ni bora na wamekuwa wakishangaa pale wanaposhindwa kupata matokeo.
“Ujue matokeo yaliyokuwa yanapatikana yanashangaza sana. Si kocha, wachezaji, viongozi, wala mashabiki, wote hatuelewi kwanini inakuwa hivyo wakati tuna timu nzuri” Alisema Mkude.
Kuhusu kocha Phiri, Mkude alisema ni ‘bonge’ la kocha kwani mara zote anakuwa kama mzazi.
“Mbali na kuwa kocha, Phiri ni kama mzazi, anawapenda wachezaji, anapenda kuelekeza, kifupi ni kocha mzuri sana. Viongozi na mashabiki wampe muda”. Alisema Mkude.
About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment