ABDULFATAH. |
Meneja wa kipa Yanga, Juma Kaseja ambaye ni Abdulfatah Saleh,ameipa
masharti timu hiyo kama inataka kipa huyo abaki kukipiga Jangwani.
Kipa
huyo, hivi sasa hana nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Mbrazili, Marcio Maximo.
Tangu msimu huu uanze, hajakaa langoni.
Maximo, kwenye kikosi chake cha
kwanza, kipa wake namba moja ni Deogratius Munishi ‘Dida’ huku Ali Mustapha ‘Barthez’, akiwa kipa chaguo la tatu
katika timu hiyo.
Abdulfatah ambaye ni mdau maarufu wa michezo nchini alisema Yanga wameshavunja mkataba na kipa huyo
kutokana na kutomkamilishia malipo ya usajili ya Sh milioni 20 ambayo
walitakiwa kuyakamilisha tangu Januari 15, mwaka huu.
Meneja
huyo anayeaminika kwa misimamo alisema ili Kaseja aendelee kuidakia Yanga, kwanza wanatakiwa kukamilisha
malipo hayo ili kuufufua mkataba lakini hata kama wakikamilisha, sharti la pili
ni lazima adake kwenye mechi tatu za kwanza za mzunguko wa pili na kama
isipokuwa hivyo, ataondoka.
Aliongeza
kuwa, kwenye usajili wa dirisha dogo litakalofunguliwa Januari, mwakani upo
uwezekano mkubwa wa kipa huyo kuihama timu hiyo baada ya masharti kuvunjwa
kwenye mkataba wake.
“Yanga
kama wanataka Kaseja abaki kuendelea kuichezea timu hiyo, basi makubaliano
yaanzeupya ikiwemo baadhi ya vipengele kurekebishwa kwenye mkataba huo.
“Moja
ya masharti tutakayowapa Yanga, ni kuhakikisha kipa huyo anapata nafasi ya
kucheza katika kikosi cha kwanza, kwa kuanziabasi acheze mechi tatu za mwanzo
za mzunguko wa pili wa ligi mara baada ya kuanza.
“Sitakuwa
tayari kumuona kipa wangu kiwango chake kikishuka mimi nikiwepo, ninataka
acheze katika kikosi cha kwanza ili kiwango chake kisishuke, kama wakitimiza
hayo, basi atabaki kuichezea
Yanga kwa makubaliano maalumu,” alisema Abdulfatah ambaye ni mmiliki wa hoteli maarufu nchini ya Sapphire Court iliyo Kariakoo jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment