MAWASILIANO

Phone. - +255 (717) 300 260 - +255 (787) 300 260

HABARI YA MUJINI

HABARI YA MUJINI
watu wa mpira

HUYU NDIYE JACKSON MAYANJA WA MSIMBAZI


Na Swabri Kachwamba
JUZI mtandao wetu ulitoa taarifa ya kocha Jackson Mayanja raia wa Uganda kutua Simba kama msaidizi wa Dylan Kerr raia wa Uingereza. Mayanja si mgeni katika soka la Tanzania kwani amewahi kuifundisha Kagera Sugar kwa zaidi ya miaka mitatu na baadaye akaenda Coastal Union ya jijini Tanga.


Katika soka la Afrika, Mayanja ni mtu mkubwa na mwenye kiwango cha juu cha kufundisha ambacho kinachangia na uzoefu alionao hasa soka la Tanzania, BOIPLUS inakuletea historia ya Mayanja wa Simba.

Mayanja aliyezaliwa Julai 27, 1969 ambaye ni maarufu kwa jina la Mia  Mia jina ambalo ni maarufu nchini Misri na Uganda. Jina hili na alipewa  wakati anacheza El Masri ya Misri mwaka 1992 wakati huo kila alichokuwa akifanya uwanjani alikuwa hakosei ndipo Wamisri walimpachika jina hilo.

Mayanja amepata elimu yake nchini Uganda aliwahi kuwa nahodha wa timi yake ya shule ya Kolokolo na baadaye alijiunga na timu ya KCC  mwaka 1987 ambako alicheza soka la ushindani ambayo alifanikiwa kuifungia mabao nane ingawa mwaka 1989 hakuweza kucheza soka kwa msimu mzima baada ya kuumia na kupelekwa Nairobi kwa ajili ya matibabu.

Baada ya kupona majeraha yake alirudi uwanjani na kuiongoza timu yake ya KCC kubeba Kombe la Kakunguru huku yeye akifunga magoli matano katika na moja goli lake muhimu alilifunga kwenye fainali dhidi ya mahasimu wao wa Villa SC  kwa ushindi wa mabao matatu.


Mwaka 1991 aliiongoza KCC kubeba Kombe la ligi huku yeye akifunga mabao 11 na kuiwezesha timu hyo kufanya vizuri mwaka uliofuata ulikuwa mzuri kwake kwani alifanikiwa kufunga mabao 23 ambayo aliyafunga kabla hata msimu haujaisha na kuamua kutimkia Misri alikojiunga na El- Masry ambako alifanikiwa kuifungia mabao nane yalichangia timu hiyo kumaliza msimu kwa kushika nafasi ya nne kwenye ligi.

Mwaka 1993, Mia mia alichaguliwa Mchezaji Bora wa ligi ya Misri na mwaka 1995 alitoka El-Masry na kujiunga na Esparance ya Tunisia ambako alicheza kwa msimu mmoja na kurudi Uganda na kujiunga na KCC aliyoifungia mabao 17 yaliyoisaidia timu hiyo kushika mafasi ya pili kwenye ligi.

Mwaka 1997, Mayanja alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora nchini Uganda na mwaka huo huo aliisaidia KCC kutwaa  ubingwa katika ligi ambapo Mayanja alitundika daluga kuichezea timu ya Taifa ya Uganda na kutimkia Oman
kukipiga klabu ya Luwi Fc ambapo mwaka 2001 alitundika daluga rasmi kucheza soka.

Baada ya kutundika daluga Mayanja akajiingiza rasmi katika kazi ya ukocha ambapo pia alijizolea umaarufu mkubwa kutokana na aina ya mpira aliokuwa akiifundisha hasa wa kugongeana pasi mfumo ambao pia alikuwa akipenda kuutumia alipokuwa Kagera Sugar yeye hupendelea kuutia mpira wa Marashi.



TIMU ALIZOFUNDISHA
URA - Uganda
KCCA - Uganda
Kagera Sugar - Tanzania
Kiyovu - Rwanda
Timu ya Taifa (U23) ya Uganda
Timu ya Taifa 'Uganda Cranes'
Coastal Union - Tanzania

MAFANIKIO
Alitwaa makombe mawili ya ligi na KCC (1991 na 1997)
Makombe  mawili ya FA akiwa na KCC (1987 na 1990) 
Makombe matatu ya Cecafa akiwa na Cranes (1990, 1992, 1996) 
Alichaguliwa Mchezaji Bora mara mbili (1993 na 1996)  

KLABU ALIZOCHEZA
KCC - Uganda
El-masry - Misri  
Esperance  - Tunisia  
Luwi FC - Oman.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment