MAWASILIANO

Phone. - +255 (717) 300 260 - +255 (787) 300 260

HABARI YA MUJINI

HABARI YA MUJINI
watu wa mpira

IBRAHIM AJIBU NDIO MCHEZAJI BORA MWEZI DISEMBA, 2015



Ibrahim Ajibu ndio mchezaji bora mwezi Disemba, 2015
Ikiwa ni tunzo ya 3 tangu kuanza kwa zoezi la kumchagua mchezaji bora wa mwezi ambapo zoezi hili lilianzishwa mwezi Septemba, 2015 likiwa na dhumuni la kuongeza morali na kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri.
Mshindi wa tunzo katika mwezi Disemba, 2015 ni Ibrahim Ajib ambapo alipigiwa kura nyingi na  mashabiki na wapenzi wa Simba na soka la Tanzania kwa ujumla kupitia simu za mkononi ambao pia wamejiunga na huduma ya Simba News pamoja na kwenye mitandao rasmi ya kijamii ya Simba Facebookwww.facebook.com/simbatanzania Twitter na Instagram @simbasctanzania.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam Rais wa Simba Evans Aveva alisema “Uongozi, wanachama na wapenzi wa Simba wanathamini mno mchango wa wachezaji katika kuifanya timu yetu ifanye vizuri, hivyo ni jambo la busara kama klabu ya kwanza Nchini Tanzania kuwa na tunzo za mchezaji wake bora kuendeleza utamaduni huu tuliokwisha uanza ambapo mchezaji wa kwanza kushinda Tunzo hii alikuwa ni Hamis Kizza akafuatiwa na Mohamed Tshabalala na sasa wapenzi, mashabiki na wanachama wamemchagua Ibrahim Ajib kuwa mshindi wa mwezi Disemba, 2015.Tunaamini kuwa Tunzo ya Mchezaji bora kwa Ibrahim Ajibu itakuwa chachu ya maendeleo katika kuendelea kucheza soka lake vizuri kwa maendeleo ya klabu na maendeleo yake binafsi katika soka”.
Akizungumza jinsi tunzo ya mchezaji bora inavyoendeshwa, Mkurugenzi Mkuu wa EAG Group ambao ni washauri na watekelezaji wa Masoko na Biashara wa Simba, Imani Kajula alisema “Wanachama na wapenzi wa Simba na wapenda michezo ndio wanaochagua mchezaji bora wa mwezi kwa kutuma jina la mchezaji wanayempendekeza kwenda kwenye namba 15460 kupitia mtandao wa Voda na Tigo’’
Simba News ni huduma iliyoanzishwa na Simba ili kuwapa wapenzi wa Simba habari mbalimbali za Simba popote pale walipo ikiwemo matokeo, majina ya wachezaji wanaocheza mechi, usajili na habari nyingine za klabu ya Simba. Kujiunga na Simba News tuma neno Simba kwenda namba 15460 kisha utaletewa ujumbe jibu kwa kutuma neon “OK” na hapo utakuwa umejiunga rasmi, Huduma hii ni maalum kwa Tigo na Vodacom.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment