Kiungo
Said Ndemla hana nafasi kikosi cha kwanza cha Simba na mara nyingi
amekuwa akiingia akitokea benchi huku Kocha Jackson Mayanja akiwatumia
zaidi Jonas Mkude na Justice Majabvi.
Kutokana
na hali hiyo, Ndemla amesema hatishwi na kuwekwa benchi kila mara kwani
anajijua anamudu kucheza nafasi tano uwanjani na ameamua kujifua zaidi
arudi first eleven.
Ndemla
alisema anamudu kucheza kiungo namba sita, kiungo mashambuliaji namba
nane, winga ya kulia na kushoto, hata mshambuliaji msaidizi, yaani namba
10.
“Sijui
kwa nini kocha hanitumii, ila yeye ndiye anayejua mahitaji ya kikosi,
mimi sihitaji kumuingilia katika hilo. Ila kwa upande wangu, kwa kuwa
nacheza nafasi tano za viungo uwanjani, nitahakikisha narejea kikosini.
“Nitaongeza
bidii katika mazoezi ili niweze kumshawishi kocha anipe nafasi ya
kuanza kikosini, ninachotaka ni kurudi kikosini, sitajali kuhusu
nafasi,” alisema Ndemla.
Kuhusiana
na hilo, Mayanja alisema: “Ndemla ni mchezaji mzuri lakini bado
naendelea kumuandaa, haiwezekani wakacheza wachezaji wote, kumbuka kuna
mifumo na falsafa katika soka.”
0 comments:
Post a Comment