Hapa nyumbani Tanzania nimeshawahi kusikia kuhusu matajiri wachache wanaofanya biashara ambao huwa hawabadili nguo zao au huwa kuna vitu wanafanya vinavyopelekea hisia za watu kuamini kwamba utajiri wao ni wa uchawi.
Mfano kuvaa nguo ya aina moja hiyohiyo kila wakati, wengine huwa wanatembelea magari mabovu kabisa lakini watoto wao na wake zao wanatembelea magari makali na wanabadilisha kila wakati, wengine tunaambiwa wanalala barazani.
Sasa hii ya tajiri wa mtandao wa kijamii wa Facebook wenye watumiaji zaidi ya bilioni moja kote duniani Mark Zuckerbeg sijui watu wataiweka kwenye kipande gani manake ameonekana mara nyingi sehemu na nyakati tofauti akiwa amevaa Tshirt moja tu ya kijivu.
Ni swali ambalo Waandishi wengi waliwahi kutamani kupata time ya kumuuliza ambapo kwa bahati nzuri kaulizwa kwenye kipindi cha maswali na majibu na akatoa jibu akiwa na tabasamu zito kabisa.
Ni swali ambalo Waandishi wengi waliwahi kutamani kupata time ya kumuuliza ambapo kwa bahati nzuri kaulizwa kwenye kipindi cha maswali na majibu na akatoa jibu akiwa na tabasamu zito kabisa.
‘Nimepata hii bahati ya kipekee kuwa kwenye nafasi niliyonayo, ninaamka kila siku na kuwahudumia zaidi ya watu bilioni moja duniani… naona sitofanya kazi yangu vizuri kama nitatumia muda wangu kwenda kutafuta/kuchagua nguo nzuri, tshirt mnayoniona nayo ni ya rangi moja lakini nilizinunua nyingi za namna hii’
‘Ni Tshirt ambayo sio moja… ninazo nyingi ila zinafanana, muda wangu mwingi nimeutenga kwa ajili ya kuhudumia watu na sio kujihudumia mimi kwenye kuchagua nguo nzuri, mavazi ni kitu kidogo sana kwangu’
0 comments:
Post a Comment