Februari
20, mwaka huu, Simba na Yanga zitacheza mechi ya raundi ya pili ya Ligi
Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, lakini maneno ya kiungo
wa Wekundu wa Msimbazi, Jonas Mkude si mazuri kwa wapinzani wao.
Mkude amesema, Yanga ikiwa na viungo wake Haruna Niyonzima, raia wa Rwanda na Thabani Kamusoko wa Zimbabwe, ijiandae kwa kipigo kwani kikosi chao kimeimarika sasa.
KAMUSOKO |
Mayanja
ameiongoza Simba katika mechi tano na kushinda zote, ambapo waliifunga
Mtibwa Sugar bao 1-0, JKT Ruvu (2-0), Burkina Faso katika Kombe la FA
(3-0), African Sports (4-0) halafu Mgambo JKT mabao 5-1.
“Hivi
sasa tupo vizuri, kazi yetu inaonekana uwanjani ambapo kila mchezaji
ana morali ya hali ya juu, hivyo timu zote tutakazokutana nazo ikiwemo
Yanga, zinatakiwa kujipanga, vinginevyo dozi itaongezeka.
MKUDE NA NIYONZIMA KAZINI.... |
“Tangu
Mayanja alipochukua mikoba ya kuifundisha timu yetu, mechi yetu ya
kwanza tulishinda bao moja, ya pili tukashinda mabao mawili, ya tatu
tukashinda tatu, ya nne tukashinda nne na ya tano tukashinda tano,
umeiona hatari hiyo kwa Yanga? Wajiandae,” alisema Mkude.
0 comments:
Post a Comment