Kiungo mshambuliaji wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi, ameongeza mkataba wa kuichezea timu hiyo
akisaini miaka miwili.
Awali,
kiungo huyo mwenye kasi kubwa uwanjani, alisaini mkataba wa miezi sita ya kuichezea
timu hiyo akitokea Yanga, akiondoka kwa mgogoro mkubwa.
Meneja wa kiungo huyo, Abdulfatah Saleh,alisema kuwa Okwi ameongeza
mkataba huo baada ya kufikia makubaliano ya pande mbili kati yao na klabu hiyo.
Abdulfatah
alisema, awali kiungo huyo alisaini mkataba mfupi wa kuichezea Simba ili kupisha kesi
iliyopo kati yake (Okwi) na Yangailiyomfungulia mashtaka kwa madai ya kukiuka makubaliano
yaliyokuwepo kwenye mkataba.
Aliongeza
kuwa, mara baada ya kumalizika kwa kesi hiyo iliyosimamiwa na Kamati yaSheria, Maadili na Hadhi za
Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ndiyo akaongeza mkataba huo
mwingine.
“Okwi
ameongeza mkataba mwingine wa kuichezea Simba, amesaini mkataba wa miaka miwili
baada ya kesi yake na Yanga kumalizika kwa TFF kumruhusu kuichezea Simba
kufuatia timu ya zamani kushindwa kutimiza makubaliano yaliyokuwepo kwenye
mkataba wake.
“Mwanzoni
alisaini mkataba wa miezi sita ili kupisha kesi hiyo imalizike, awali alisaini
mkataba huo kwa hofu ya kushindwa kesi hiyodhidi ya Yanga,” alisema Abdulfatah.
0 comments:
Post a Comment