Bila ya kuwa na mshambuliaji nyota wa Simba, Emmanuel Okwi, timu ya taifa ya Uganda imefanikiwa kuiangusha Ghana kwa kuichapa bao 1-0.
Okwi aliondolewa katika kikosi hicho baada ya kuwa majeruhi lakini kocha wake akasema ana nafasi ya kurejea The Cranes.
Uganda inanolewa na kocha wa zamani wa Yanga, Sredojevic Milutin 'Micho'. Bao la Uganda lilifungwa na Savio Kabugo kwa kichwa katika dakika ya 10 akiunganisha mpira wa kona.
Katika mechi hiyo iliyochezwa leo kwenye Uwanja wa Mandela mjini Kampala, Uganda ilipata bao lake katika kipindi cha kwanza.
Hata hivyo, Ghana iliyokuwa inaongozwa na nahodha Andre Ayew anayekipiga nchini Ufaransa, ilijitahi kuipa Uganda wakati mgumu.
Ushindi huo unaifanya Uganda ijiweke katika nafasi nzuri ya kucheza Kombe la Mataifa Afrika.
Timu nyingine ya Afrika Mashariki na Kati ilikuwa Sudan ambayo ilikuwa ugenini dhidi ya Afrika Kusini.
Wenyeji Bafana Bafana wameibuka na ushindi wa maao 2-1.
MATOKEO MENGINE:
Malawi 2-0 Mali
0 comments:
Post a Comment