MAWASILIANO

Phone. - +255 (717) 300 260 - +255 (787) 300 260

HABARI YA MUJINI

HABARI YA MUJINI
watu wa mpira

DAN SSERUNKUMA AMENG’ARA KATIKA TUZO ZA LIGI KUU YA KENYA

sere
MCHEZAJI anayetajwa kwenye orodha ya nyota wanaowaniwa na Klabu ya Simba katika usajili wa dirisha dogo kipindi hiki, Mganda Dan Sserunkuma ameng’ara katika tuzo za Ligi Kuu ya Kenya zilizotolewa jijini Nairobi, Kenya jana usiku.
Kwa mujibu wa Mtandao wa futaa.com, kiungo wa Sofapaka, Anthony Ndolo alitwaa mataji mawili makuu; mchezaji na kiungo bora wa mwaka huku huku kocha wake Mganda Sam Timbe akimaliza wa pili nyuma ya Mike Mururi wa Chemelil Sugar katika kipengele cha kocha bora.
Mabingwa Gor Mahia kwa upande wao walijivunia ushindi wa David Owino na Ronald Ngala kwenye safu ya beki bora na mwenyekiti bora mtawala na kisha timu hiyo kuibuka ya pili kwenye timu yenye nidhamu (mchezo wa kiungwana) msimu huu.
Kiungo wa Gor na Timu ya Taifa ya Uganda (Cranes), Geoffrey Kizito naye alitangazwa namba mbili katika tuzo za kiungo na mchezaji bora huku mlinda mlango Jerim Onyango akimaliza wa pili kwenye tuzo za kipa bora wa mwaka, nyuma ya Jairus Adira wa Chemelil Sugar.
Kwenye tuzo nyingine, Sserunkuma ambaye mwaka jana alikuwa Mchezaji Bora wa Ligi ya Kenya, alitwaa taji la daluga la mfungaji bora kwa kucheka na nyavu mara 16 msimu huu.
Hamisi Mwinyi wa Chemelil Sugar akizawidiwa mchezaji mwenye mchezo bora naye William Muluhya wa Mathare United akaibuka timu meneja bora mbele yake Amenipa Bigisho na George Maina wa Sofapaka na Thika United.
Waamuzi wasimamizi wa mechi pia hawakuachwa nyuma kwani Peter Waweru na Steven Oduor walitangazwa refa na msaidizi wake bora mtawala.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF), Sam Nyamweya na Mwenyekiti wa Ligi Kuu, Ambrose Rachier miongoni mwa viongozi wengine.
TUZO ZA WACHEZAJI/MAKOCHA/VIONGOZI BORA 2014
Mchezaji Bora: Ekaliani Ndolo (Sofapaka)
Kipa Bora: Jairus Adira (Chemelil Sugar)
Beki Bora: David Owino (Gor Mahia)
Kiungo Bora: Ekaliani Ndolo (Sofapaka)
Daluga la Mfungaji Bora: Dan Sserunkuma (Gor Mahia)
Mchezo Bora: Hamisi Mwinyi (Chemelil Sugar)
Timu yenye Mchezo Bora: Muhoroni Youth
Kocha Bora: Mike Mururi (Chemelil Sugar)
Timu Meneja Bora: William Muluhya (Mathare United)
Mwamuzi Bora: Peter Waweru
Refa Msaidizi Bora: Steven Oduor
Mwenyekiti Bora: Ronald Ngala (Gor Mahia)

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment