Gwiji la soka kutoka nchini Brazil, Pele amekimbizwa hospitali na kulazwa kutokana na matatizo ya mkojo.
Imeelezwa Pele alifikishwa hospitali jana ikiwa ni mara ya pili kufikishwa hospitali kutokana na matatizo hayo.
Mkali huyo mwenye miaka 74 aliyetangazwa mchezaji wa karne wa Fifa, bado amelazwa katika hospitali ya Albert Einstein Hospital jijini Sao Paulo.
Pele alikuwa amelazwa kwenye hospitali hiyo siku 10 zilizopita baada ya kufanyiwa upasuaji ili kuondoa mawe kwenye figo lake.
Taarifa zinasema anaendelea vizuri, ingawa kumekuwa na hofu kwa mashabiki wa soka nchini humo.
0 comments:
Post a Comment