MAWASILIANO

Phone. - +255 (717) 300 260 - +255 (787) 300 260

HABARI YA MUJINI

HABARI YA MUJINI
watu wa mpira

MKUDE ASAINI KWA MILIONI 60 MIAKA MIWILI SIMBA SC

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
KIUNGO Jonas Gerald Mkude amesaini Mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea Simba SC na kusema; “Bado nipo sana Msimbazi”.
Akizungumza baada ya kusaini Mkataba huo mbele ya Waandishi wa Habari, katika ukumbi wa Silver Pippe, Kawe, Dar es Salaam Mkude amesema kwamba amesaini klabu hiyo baada ya kufikia kiwango cha fedha alichotaka.
Ingawa Mkude mwenyewe hakusema ni kiasi gani amepewa, lakini habari ambazo BIN ZUBEIRY imezipata zinasema kiungo huyo amepewa Sh. Milioni 60, ingawa mwenyewe alianzia Milioni 80.
Jonas Mkude (katikati) akisaini Mkataba wa Simba SC. Kulia ni Rais wa Simba SC, Evans Aveva na kushoto Hans Poppe


“Nafurahi kusaini Simba SC, klabu ambayo imenikuza kisoka tangu timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 hadi leo, nawaahidi wana Simba SC kuendelea kufanya kazi kwa juhudi ili kuiletea mafanikio klabu yangu,”amesema.
Lakini Mkude hakutaka kuzungumzia kuhusu klabu za Yanga na Azam FC ambazo ziliripotiwa kumuwania kabla ya kusaini Mkataba huo mpya, alisema; “Mambo ya mpira unaweza kuangukia popote, nadhani huu si wakati wake kuzungumzia Azam au Yanga,”.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba wameamua kumuongezea Mkataba mchezaji huyo wa nafasi ya kiungo cha ulinzi, baada ya kugundua wapinzani wao, Yanga na Azam walikuwa wanamghasi.
Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akamtania kidogo Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji; “Baada ya sisi kumsaini Okwi (Emmanuel), Manji alisema anaweza kusajili wachezaji wote wa Simba akawaweka Coco Beach. Sasa hiyo kauli ndiyo imemkosesha Mkude, kwa sababu yeye hakutaka kwenda mchangani, alitaka kucheza mpira uwanjani, ndiyo maana amesaini tena Simba SC,”alisema.
Mkude ni mchezaji aliyeibuliwa katika mfumo wa soka ya vijana wa Simba SC kabla ya mwaka wa 2011 kupandishwa kikosi cha kwanza ambako hivi sasa ni tegemeo. Alikuwa amebakiza miezi sita katika mkataba wake wa awali
12Nov2014
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment