HANS POPPE. |
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema baba wa kiungo wa Yanga, Simon Msuva anapaswa kukaa kando katika suala la mwanaye.
Hans Poppe ambaye yuko nchini Ujerumani, amesema mzazi huyo anapaswa kukaa kimya na kuwaacha Simba wamalizane na Yanga na mwanaye.
MSUVA AKISHANGILIA NA WENZAKE BAADA YA KUIFUNGUA YANGA BAO. |
“Baada ya hapo yeye atampelekea dau baba yake halafu atafurahia.
“Sidhani kama kuna mzazi anaweza kumzuia mwanaye asipate fedha,” alisema Hans Poppe.
Kuhusiana na suala la kupeleka barua ya kumtaka Msuva, Hans Poppe alisema wataipeleka mara baada ya kufunguliwa kwa dirisha dogo.
Lakini Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu yeye alisema bado hawajapokea barua hiyo ya Simba.
“Hadi sasa hatujaona barua yoyote kuhusiana na Msuva,” alisema.
0 comments:
Post a Comment