KIBADENI WAKATI AKIINOA SIMBA... |
Kocha wa zamani wa Simba na Kagera Sufar, Abdallah Kibadeni amesema atafungua shule ya michezo itakayojumuisha ile ya kikapu na netiboli.
Kibadeni amesema atafungua akademi hiyo katika eneo la Chanika jijini Dar es Salaam na mchezo utakaoanza kufundishwa ni soka.
“Soka ni namba moja ndugu yangu kwa kuwa mimi ni mwalimu wa mchezo huo. Lakini kadiri siku zinavyosonga mbele, tutafungua na michezo mingine.
“Mfano netiboli, kikapu. Hii ni kuifanya kuwa shule ya michezo yote ile ambayo inaweza kutoa vijana na kuendeleza vipaji vyao,” alisema.
Kibadeni alipoulizwa kuhusiana na suala la kufundisha timu za Ligi Kuu Bara, alisema.
“Kwa kweli acha nipumzike, presha ni kubwa. Watu hawaridhiki hata kidogo.”
0 comments:
Post a Comment