KALI (WA PILI KUSHOTO) WAKATI AKIITUMIKIA AZAM FC AKIWA NA KOCHA STEWART HALL (KUSHOTO). |
Kocha Msaidizi wa Azam FC, Kali Ongala ameachia ngazi.
Ongala ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mwanamuziki maarufu nchini, Dk Remmy Ongala ameachia ngazi kwa kuwa anakwenda masomoni.
Taarifa za awali zilieleza kwamba Kali aliamua kuachia ngazi kutokana na kuona haridhishwi na mambo fulani.
Lakini msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi akaiambia SALEHJEMBE kuwa ulikuwa ni uamuzi wake tokea mapema.
“Kali aliomba mapema kwamba anataka kuachia ngazi. Halikuwa suala la matatizo au vinginevyo.
“Ukweli ni kwamba anakwenda kusoma nchini Uingereza,” alisema Jaffar.
Kali ni mshambuliaji wa zamani wa Yanga mwenye uraia wa Uingereza, mama yake mzazi pia ni Mwingereza.
0 comments:
Post a Comment