Maelfu ya wakazi wa mji wa Shinyanga na maeneo ya jirani waliojitokeza jioni ya jana katika viwanja vya mahakama ya mwanzo Nguzo Nane mjini Shinyanga katika mkutano mkubwa wa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA) Taifa ndugu
Halima Mdee ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kawe.

Pamoja na mambo mengine viongozi mbalimbali wa chama hicho walisisitiza umuhimu wa kujiandikisha katika daftari la wapiga kura na kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa hapo Desemba 14, 2014..


Viongozi mbalimbali wa CHADEMA ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa wakiwa jukwaa kuu jioni ya jana mjini Shinyanga.



Mzee Robert Ng'welo akikabidhi kadi ya CCM kwa Halima Mdee na kupewa kadi ya CHADEMA jioni ya leo.Mdee alisema CHADEMA ni chama cha Watanzania bila kujali umri!


Maelfu ya wananchi wakifuatilia mkutano wa CHADEMA jioni ya jana mjini Shinyanga.

- Picha: Kadama Malunde, Shinyanga