Taarifa ambayo imeripotiwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ni kuhusu watu wanne kufariki kutokana na ajali ya Helikopta inayomilikiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, yenye namba 5HTWA kuanguka katika eneo la Kipunguni B, Ukonga Dar es salaam.
Akizungumza na kituo cha ITV Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kutoa taarifa kamili juu ya tukio hilo muda mfupi ujao.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu@LazaroNyalandu ameandika hivi; “Naelekea Dar kutokea Dodoma kwenda kwenye eneo la tukio la ajali ili kuwapa pole wafiwa. Nitazidi kuwafahamisha.”
About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment