Mshambuliaji Paul Kiongera hatimaye amerejea na kuungana na wenzake na kufanya nao mazoezi ya pamoja.
Kiongera raia wa Kenya aliumia katika mechi ya kwanza tu ya Ligi Kuu Bara alipoingia wakati Simba ikiivaa Coastal Union.
Kiongera leo aliungana na wachezaji wa Simba kwenye Gym na kufanya nao mazoezi pamoja.
Baadaye chini ya Kocha Msaidizi, Selemani Matola alingozana nao tena hadi kwenye Uwanja wa TCC Chang’ombe ambako walifanya mazoezi pamoja.
0 comments:
Post a Comment