MAWASILIANO

Phone. - +255 (717) 300 260 - +255 (787) 300 260

HABARI YA MUJINI

HABARI YA MUJINI
watu wa mpira

KAWEMBA CEO MPYA AZAM FC

Kawemba, aliyeng’ara katika uongozi wa aliyekuwa rais wa TFF, Leodegar Tenga, hakupewa mkataba mpya na uongozi mpya wa TFF chini ya Rais wake Jamal Malinzi baada ya mkataba wake kumalizika Desemba mwaka jana licha ya kuligharimu Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) mamilioni ya shilingi katika kumwongeza ujuzi wa masuala ya utawala wa soka.
saa
Mwenyekiti wa Azam FC, Said Muhammad amemtambulisha rasmi leo Kawemba mbele ya wachezaji na viongozi wa Azam FC kwenye makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo Chamazi jijini Dar es Salaam, baada ya mazoezi ya asubuhi.
“Nafurahi kupata nafasi hii, ni fursa nyingine tena ya kupata uzoefu mwingine katika uongozi wa soka baada ya kufanya kazi kwa mafanikio TFF,” Kawemba amesema baada ya kutambulishwa jana.
Muhammad amesema Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC imefikia hatua ya kuajiri Mtendaji Mkuu ili kurahisisha uendeshaji ndani ya klabu kwa lengo la kutafuta ufanisi zaidi.
Kawemba amesema anatarajia kupata ushirikiano mzuri kutoka kwa Bodi, Menejimenti na wafanyakazi wote wa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na wawakilishi wa Tanzania Bara katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika mwakani.
“Nimekuja hapa kusaidia kusukuma mbele gurudumu la maendeleo la Azam FC, ninatarajia ushirikiano wa wote,”amesema.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment