Wakati Wanayanga wakiwa na furaha kutokana na kuwasili kwa kiungo Mbrazili, Emerson de Oliveira Roque ambaye yupo mbioni kusaini mkataba wa kuitumikia Yanga, upande wa pili kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude, ameupokea tofauti ujio wa Mbrazili huyo.
Jonas ambaye amesaini mkataba mpya wa kuitumikia timu hiyo, ameuliza kama kweli Emerson anaweza kufananishwa naye baada ya habari hiyo kutoka gazetini.
Akiwa katika mazoezi ya gym yanayofanyika kwenye Gym ya Chang’ombe jijini Dar, Mkude alisikika akimponda mchezaji huyo na kusema kuwa mchezaji bora siku zote huonekana uwanjani na si kupambwa katika vyombo vya habari.
“Huyu jamaa anavyopambwa kabla hata hatujamuona uwanjani ni kweli ana uwezo au walewale tu! Mimi ninamsubiri uwanjani maana wameonyesha hapa eti anaweza kunifunika, mhhh! tusubiri kuona,” alisema Mkude.
Yanga imemshusha nchini Emerson ili kuziba nafasi baada ya kuachana na Mbrazili mwingine, Geilson Santos ‘Jaja’ aliyeamua ‘kuomba poo’ baada ya maji kuwa mazito kwake katika msimu wa kwanza wa Ligi Kuu Bara.
0 comments:
Post a Comment