Danny Mrwanda,mshambulizi wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ameondoka nchini kwenda nchini Vietnam kucheza soka la kulipwa.Mchezaji huyu wa zamani wa AFC Arusha na Simba SC amefunga mabao manne katika michezo saba ya ligi kuu Tanzania Bara msimu huu akiwa na timu ya Polisi Morogoro.
Mrwanda amewahi kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Al Tadamon ya Kuwait, 2008-09, kabla ya kurudi Simba na kucheza kwa muda mfupi katika msimu wa 2009/10. Simba ilimuuza kwa mara ya pili safari hii wakimuza kwa klabu ya Dong Tam Long An ya Vietnam ambako alicheza hadi mwaka 2011 alipojiunga na Hoang Anh Gia Lai pia ya nchini humo.
Bao lake dhidi ya Simba ambalo lilikuwa ni la kusawazisha katika mchezo kati ya Polisi Morogoro na timu yake hiyo ya zamani lilikumbusha watu kuhusu kipaji cha mchezaji huyo ambaye alitemwa na Simba muda mfupi baada ya kusaini mkataba wa kuichezea timu hiyo katikati ya mwaka, 2012. Mrwanda, 31 alitumia vizuri pasi ya kunyeza iliyopigwa na Salum Machaku kufunga bao la kiufundi ambalo liliipatia pointi ya kwanza Polisi msimu huu.
Akiwa ameifungia timu yake mabao manne huku bao la mwisho akifunga katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons mwishoni mwa wiki, Mrwanda amekwenda nchini Vietnam kwa mara nyingine kucheza soka la kulipwa. “ Danny ameondoka leo kwenda nchini Vietnam” anathibitisha mmoja wa wachezaji wa zamani wa timu hiyo ambaye kwa sasa ni mmoja wa viongozi waandamizi wa timu hiyo.

About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment