MONDAY, NOVEMBER 10, 2014
MWANAMUZIKI MKONGWE WA TWANGA PEPETA,AMIGOLAS AZIKWA MAKUBURI YA KISUTU JIJINI DAR LEO
Mwimbaji na mtuzni, Ali Choki, akiwa na uso wa huzuni wakati wa mazishi ya AMIGOLAS, ambaye kipindi gulani walikuwa bendi moja ya Twanga Pepeta |
Waombolezaji wakiwemo wasanii maarufu, wakiwa kwenye mazishi. |
Waombolezaji na wasanii wakiwemo wanamuziki wakiwa nyumbani kwa marehemu AMIGOLAS, kabla ya mzishi yake.PICHA KWA HISANI YA K-VIS BLOG |
MONDAY, NOVEMBER 10, 2014 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG ~ MTUMIE RAFIKI YAKO , MAONI: 0
AKUDO IMPACT, MASHUJAA MUSIC NA JAHAZI MODERN TAARAB KUSINDIKIZA UZINDUZI WA ALBAM YA TARSIS MASELA
BENDI mbili za muziki wa dansi, Akudo Impact, Mashujaa Music pamoja na kundi la mahiri la muziki wa taarab la Jahazi Modern Classic vitasindikiza uzinduzi wa albamu mpya wa msanii, Tarsis Masela (pichani katikati) unaotarajiwa kufanyika Novemba 21 kwenye ukumbi wa Ten Lounge jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es salam leo , Meneja wa mwanamuziki huyo, Ray Matata, alisema kuwa maandalizi ya uzinduzi huo yamekamilika na bendi zote tatu zimethibitisha kutoa burudani siku ya uzinduzi huo.
Matata alisema kuwa wameandaa onyesho ambalo litakuwa ni historia katika muziki wa dansi hapa nchini. Masela alisema kwamba amejiandaa kuwapa mashabiki wa dansi wa Tanzania burudani yenye ubora na lengo lake ni kuonyesha kipaji chake katika sanaa ya muziki.
“Huu ni mwaka wa saba niko Tanzania, nimejiandaa kuwapa burudani bora mashabiki wa muziki na kuwaachia zawadi ambayo hawataisahau kwenye tasnia ya muziki wa dansi,” alisema Masela.
Aliongeza kuwa albamu yake anayotarajia kuizindua ina jumla ya nyimbo nane na itajulikana kwa jina la Acha Hizo. Alizitaja nyimbo zinazounda albamu hiyo kuwa ni pamoja na Tabia Mbaya, Mwiko, Chaguo Langu, Tusiachane, Penzi Langu Limezidi Asali, Vidole Vitatu na Nimevulimia.
Alieleza kwamba katika albamu hiyo ameshirikisha wasanii wa aina mbalimbali ili kuifanya iwe na ubora kwa kupendwa na wadau wa rika tofauti. Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa bendi ya Mashujaa, Maximillian Luhanga, alisema kwamba wamekubali kusindikiza uzinduzi wa albamu hiyo kwa kuheshimu kipaji cha Masela na kutaka kuendelea wasanii wa muziki wa dansi.
Luhanga alisema kwamba hiyo itaondoka ile dhana ya wasanii wa dansi hawapendani na amewataka wanamuziki wengine kufuata nyayo za msanii huyo mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
MONDAY, NOVEMBER 10, 2014
RAIS WA BUNGE LA SADC NA SPIKA WA BUNGE LA TANZANIA MHE. ANNE MAKINDA ASHIRIKI MISA MAALUM YA KUMWOMBEA ALIYEKUWA RAIS WA ZAMBIA MAREHEMU MICHAEL SATA KATIKA VIWANJA VYA BUNGE LA ZAMBIA MJINI LUSAKA LEO
Mwili wa aliyekuwa Rais wa Zambia marehemu Michael Sata ukiwasili katika viwanja vya Bunge la Zambia leo tayari kwa misa Maalum iliyoandaliwa kabla ya mazishi kufanyika hapo kesho.
Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwasili katika viwanja vya Bunge la Zambia tayari kushiriki Misa Maalum ya Kumwombea aliyekuwa Rais wa Zambia Mhe. Michael Chilufya Sata kabla ya maziko yake kufanyika hapo kesho.
Aliyekuwa Rais wa Serikali ya Awamu wa Zambia Mhe. Lupia Banda akimpokea Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda alipowasili katika viwanja vya Bunge la Zambia tayari kushiriki Misa Maalum ya Kumwombea aliyekuwa Rais wa Zambia Mhe. Michael Chilufya Sata kabla ya maziko yake kufanyika hapo kesho.
Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akisalimiana na Rais wa Kwanza wa Zambia Dkt. Kenneth Kaunda mara baada ya Kuwasili katika Viwanja vya Bunge kushiriki Misa hiyo.
About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment