Mshambuliaji nyota wa Yanga, Mrisho Ngassa leo amefunga ndoa na binti ‘mkalee’ aitwaye Ladhia.
Ndoa hiyo imefungwa nyumbani kwao Ladhia aneo la Tegete jijini Dar es Salaam.
Kipa Juma Kaseja ndiye alikuwa akimsindikiza Ngassa katika shughuli hiyo iliyofana.
Hiyo ni ndoa ya pili kwa Ngassa ambaye ameamua kufunga ndoa baada ya kuachana na mkewe wa kwanza, miaka mitatu iliyopita.
0 comments:
Post a Comment