MAWASILIANO

Phone. - +255 (717) 300 260 - +255 (787) 300 260

HABARI YA MUJINI

HABARI YA MUJINI
watu wa mpira

Ripota wangu wa Uganda amefatilia mwanzo mwisho kuhusu yule Housegirl aliepiga mtoto

Uganda PoliceKuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita kulikua na stori imesambaa sana kwenye mitandao ya kijamii kama instagram, facebook na twitter kuhusu msichana wa kazi ambae alitegeshewa na Baba mwenye nyumba kamera nyumbani na baadae video iliyorekodiwa ikamuonyesha akimpiga mtoto wa mwenye nyumba.
Baadae zilitoka stori mbalimbali kwamba Mtoto mwenyewe ambae ana umri wa miaka miwili amefariki, ni stori ambazo ziliambatana na taarifa nyingine zisizo na ukweli ambazo ripota wa TZA (millardayo.com na AyoTV) Uganda Bill The African amefatilia moja baada ya nyingine kama ifuatavyo.
  • Msichana huyu wa kazi anaitwa Tumuhairwe ana umri wa miaka 22 na sio 25 kama ilivyoripotiwa ambapo ana siku 26 tu toka aanze kufanya kazi kwenye familia ya mtoto huyo.
ugando housegirl- Kwa sasa yuko rumande kwenye gereza la Luzira Uganda na atafunguliwa mada ya kutaka kuua.
–  Unaambiwa haya yote yasingejulikana kama Polisi isingemkamata baba mzazi wa mtoto huyu, yani baba alipoona ile video ndio akampiga Msichana huyu wa kazi ambae baada ya kipigo alikwenda kumshitaki baba wa mtoto Polisi.
  • Polisi walipomchukua Erick Kamanzi (Baba wa mtoto) nyumbani kwa ke na kumfikisha Polisi ambako alieleza sababu za kumpiga Msichana huyu na kuwaonyesha Polisi hii video hapa chini ambayo ni ya tukio la mtoto wake kupigwa.
uganda 3- Baada ya hapo Polisi ndio wakamwachia na kumkamata Msichana huyu wa kazi.
  • Erick ambae ndio baba mzazi wa mtoto huyu amesema wanashukuru Mungu mtoto kuwa hai bila matatizo na sasa mtoto amekua karibu na baba yake zaidi.
  • Tarehe 8 December ndio atapandishwa Mahakamani kusomewa mashitaka yake.
  • November 24 2014 Waziri wa mambo ya vijana wa Uganda aliitembelea familia ya mtoto huyu baada ya watu kuanza kusambaza habari kwamba mtoto huyu alifariki, taarifa ambazo sio za kweli.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment