Mlinzi-kiungo wa zamani wa Simba SC na timu ya Taifa ya Tanzania, Said Sued amemmwagia sifa kocha wake Jamhuri Kiwhelo Julio na kumtaja kama ‘ kocha mwenye thamani kubwa wachezaji wa Kitanzania’. Sued ambaye kwa sasa anaichezea timu ya daraja la kwanza ya Mwadui FC ya Kahama, Shinyangs amesema hayo wakati alipofanya mazungomzo ya mtandao huu.
“ Julio ni kocha ambaye anapenda sana vipaji, hapendi kuona mchezaji mzuri akipotea kwa sababu ya maneno ya watu” anasema Sued ambaye alikuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi ( miaka 17) kucheza katika ligi kuu mwaka 2001 aliposajiliwa na Simba akiwa mwanafunzi wa kidato cha pili. Alijiunga Simba na kushinda taji la kwanza la ligi kuu mwaka huo.
Pia mlinzi huyo wa pembeni ( kulia au upande wa kushoto) alishinda mataji mengine matatu katika miaka ya 2003, 2004, na 2007 akiwa na Simba kabla ya kuachana na timu hiyo.
“ Tuna uhakika Mwadui itapanda na kucheza ligi kuu msimu ujao, chini ya Julio tumekuwa na mwendo mzuri, tunapambamna kuipandisha timu hii kwa uwezo wa mola tutapanda”. Mwadui imekusanya wachezaji wengi mahiri katika kikosi hicho. Sued na kaka yake Salum Sued ‘ Kussi’ pia ni miongoni mwa mastaa ambao wanapiga kazi na Julio katika timu hiyo.
About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment