Kocha Msaidizi wa timu taifa ya Myanmar, Milovan Cirkovic amesema anaendelea vizuri na kazi yake na sasa kikosi cha timu yake kimesafiri hadi Singapore kinaposhiriki mashindano ya Suzuki Cup.
Akizungumza kutoka Singapore, Milovan aliyewahi kuinoa Simba kwa vipindi viwili tofauti amesema tayari wamecheza mechi moja dhidi ya Malaysia na kutoka sare ya bila mabao.
"Katika kundi letu, timu nyingine ni wenyeji Singapore na Thailand. Ni gumu sana, lakini tunafanya kila jitihada," alisema Milovan.
"Ila kuna kundi la pili lina timu nne pia, lakini wao wako Vietnam ambako wanacheza kule.
"Maisha huku ni mazuri, tunaendelea na kazi vizuri pia, lengo ni kutaka kuleta mabadiliko."
0 comments:
Post a Comment