Azam FC imemsaini limnzi wa kati wa kimaifa wa Ivory Coast , Serge Paschal Wawa ambaye amemaliza mkataba wake na klabu bingwa ya CECAFA, El Merreikh ya Sudan. Simba SC imerefusha mkataba na kiungo wake Jonas Mkude. Kila timu imekuwa ikijiimarisha hasa wakati huu ushindani katika ligi kuu Tanzania Bara ukiwa wa kiwango cha juu.
“ Tumemsainisha Mkude kwa sababu walikuwa wakimsumbua, wakifikiria kwamba mkataba wake unakwisha baada ya miezi sita na miezi sita haijatimia kwa sababu mkataba wake wa awali unamalizika mwezi wa sita mwakani, na leo hii ni Novemba. Wale wote waliokuwa wakizungumza naye ni makosa, hakuna mkataba wa mchezaji ndano ya Simba unaoisha ndani ya miezi sita. Nathibitisha kuwa Mkude ameongeza mkataba wa miaka miwili” ni maneno ya Zacharia Hans Poppe, mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu ya Simba.
Simba imemuongeza mkataba Mkude ambaye ametokea timu ya vijana ya klabu hiyo, ni jambo la kupendeza kuona klabu ikiwalinda wachezaji wake, kwa kitendo cha kumsaini tena Mkude kwa miaka miwili zaidi ni sawa na kuonesha kuwa timu hiyo haipo tayari kuwapoteza wachezaji wake muhimu. Lakini kutangaza hadharani kuwa watapeleka ofa ya kumsaini kiungo-mshambulizi wa mahasimu wao Yanga SC, Saimon Msuva ni sawa na kuamsha vita baina ya timu hizo.
Msuva bado ni mchezaji mwenye mkataba na Yanga, lakini Sima inataka kuchukulia mwanya wa ‘ habari za Msuva ni Simba’ kumshawishi mchezaji huyo ambaye ni muhimu zaidi katika kikosi cha Yanga. Kupeleka ofa ni jambo lenye kuonesha wazi kuwa viongozi wa klabu hiyo wanajifunza namna ya kufanya usajili ulio wa haki na kuachana na ‘ usajili wa njia za panya’. Yanga watakuwa na chaguo la kukubali ofa itakayopelekwa kwao ama wanaweza kuitupilia mbali kama haitakuwa na maslai.
“ Tutawandikia barua Yanga ya kuitaji kumsajili Msuva” alisema, Poppe. Kocha wa Yanga, Marcio Maximo amesema kuwa, ataongoza baadhi ya wachezaji katika nafasi ya kiungo wakati wa dirisha dogo, maana yake kuwa anahitaji kuongeza nguvu zaidi katika kikosi chake. Hakutakuwa na nafassi ya Msuva kuondoka Yanga kwa hali yoyote wakati huu. Kama ambavyo Simba imeona umuhimu wa kuendelea kuwa na mchezaji kama Mkude, Yanga pia watahitaji kuona mchezaji wao bora anaendelea kubaki katika timu yao.

Thamani ya wachezaji hao wawili haipo katika suala la pesa, umuhimu katika vikosi vyao, malengo ya wachezaji wenyewe. Kama Mkude ametengeneza maisha yake kupitia Simba, ni hivyo pia kwa Msuva, maisha yake ya soka yamebebwa na Yanga. Ni kijana ambaye anaingia katika ushindani wa soko la usajili kuanzia usajili huu wa dirisha dogo. Thamani ya Msuva na Mkude ni kubwa sana, Mkude kasaini tena Simba, itakuwa hivyo kwa Msuva na Yanga kwa sababu wote ni wachezaji walio katika mipango ya klabu zao.
About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment