Bobbi
Kristina Brown ,mtoto wa marehemu Whitney Houston ambaye alikuwa gwiji
wa muziki wa R&B ,amefariki dunia baada ya kupoteza fahamu kwa muda
wa miezi sita tangu alipokutwa taabani kwenye bafu lake na pindi
alipofikishwa hospitalini na kukutwa na matatizo kwenye ubongo.
Bobbi amekufa akiwa na umri wa miaka 22,huku akivutiwa kuwa muigizaji na muimbaji mahiri na mwenye ubora wa aina yake.
BBC
SWAHILI wameripoti kwamba, Msemaji wa familia Kristen Foster amesema
Bobbi amefariki akiwa amezungukwa na familia yake ,''hatimaye yuko
salama sasa kwenye mikono ya Mwenyezi Mungu,tunawashukuru wote
walioungana nasi katika maombi na kuonesha upendo kwa miezi michache
iliyopita''.
Bobbi
ambaye alikuwa amepoteza fahamu tangu akutwe ameanguka kwenye bafu lake
panapo tarehe 31 januari mwaka huu na kuwekwa kwenye matibabu huku
akiwa amekosa ufahamu na mpaka kifo chake kumkuta alikuwa hajapata
fahamu bado.Inakumbukwa kuwa miaka mitatu iliyopita mama yake
Bobbi,alikutwa pia kwenye bafu lake amepoteza fahamu baada ya kupitliza
kiwango cha dawa za kulevya na pombe mwishowe kufa.
Bobbi alikuwa mtoto pekee wa Whitney Houston na Bobby Brown,magwiji wa muziki wa miondoko ya R &B.
0 comments:
Post a Comment