Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi ameshinda
tuzo ya mchezaji bora wa dunia (Ballon d’Or award ) kwa mwaka 2015
ikiwa ni mara ya tano anatwaa tuzo hiyo.
Messi, 28, amepata asilimia 41.33 ya kura zote zilizopigwa akifuatiwa
na mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo mwenye asilimia 27.7
wakati Neymar wa Barcelona akiambulia asilimia 7.86 ya kura zote.Messi na Ronaldo kwa pamoja wameshinda tuzo hiyo mara nane.
Kiungo wa United States Carli Lloyd ambaye alifunga bao tatu kwenye fainali ya kombe la dunia ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa upande wa wanawake.
Kocha wa USA Jill Ellis amempiku kocha wa England Mark Sampson kwenye tuzo ya kocha bora wa soka la wanawake.
Kikosi bora cha FIFA (FIFA/Fifpro World XI)
Real Madrid na Barcelona ndiyo clab zenye wachezaji wengi kwenye kikosi hicho zikiwa zimetoa wacheza wanne kwenye timu hiyo bora ya mwaka.
Golikipa wa Manuel Neuer wa Bayern Munich ndiye mchezaji pekee anayewakilisha ligi ya Ujerumani. EPL ndiyo ligi pekee kati ya ligi tano za juu za Ulaya kutotoa mwakilishi hata mmoja kwenye kikosi hicho.
Kocha wa Barcelona Luis Enrique ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwaka baada kukiongoza kikosi chake kutwaa mataji matano kati ya sita ndani ya mwaka 2015 lakini yaliyompa heshima kubwa ni mataji matatu (treble) Champions League, La Liga and the Copa del Rey.
Luis Enrique amemshinda kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola ambaye alikuwa wapili wakati mshindi wa Copa America Jorge Sampaoli akimaliza nafasi ya tatu.
Goli bora la mwaka (Puskas award)
Mchezaji wa Atletico Goianiense Wendell Lira ameshinda tuzo ya goli bora la mwaka.
Hii ni Orodha ya washindi wa tuzo ya Ballon d’Or tangu mwaka 2003 mpaka 20014 ambapo mwaka 2015 imenyakuliwa na Messi.
0 comments:
Post a Comment