MAWASILIANO

Phone. - +255 (717) 300 260 - +255 (787) 300 260

HABARI YA MUJINI

HABARI YA MUJINI
watu wa mpira

MZUNGU WA SIMBA ATOA MPYA ZENJI, AWAKIMBILIA MASHABIKIK NA KUTOA SOMO



Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr, amewashangaza mashabiki wa soka visiwani hapa, baada ya kuacha kuwafanyisha mazoezi wachezaji wake na kukimbilia jukwaani kuwaelewesha mashabiki.

Kikosi cha  Simba juzi kilifanya mazoezi yake kwenye Uwanja a Amaan lakini mashabiki wa timu hiyo waliohudhuria walionekana kutofurahia mbinu ambazo kocha huyo alikuwa akizitumia, wakaanza kumpigia kelele, ndipo alipoamua kupanda jukwaani na kuzungumza nao kwa lengo la kuwaelewesha.
Kerr, raia wa Uingereza, aliwaeleza mashabiki wa timu hiyo kuwa anatengeneza kikosi chenye washambuliaji wenye uwezo wa kupiga mashuti.

Programu ya mazoezi ya kocha huyo, ilikuwa ni kupanga washambuliaji watano na mabeki wanne wanaocheza kwa kuchuana huku wengine wakisubiri na wanapomaliza muda wao, wanaingia wengine.

Kwa upande wa mashabiki, walisema haijawahi kutokea kuona kitendo hicho Zanzibar, kocha kutoka nje ya uwanja na kwenda kuwafahamisha mashabiki jinsi anavyofundisha.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment