Kazimoto (kulia) akiwa na Rais wa Simba, Evans Aveva
Hatimaye
kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Mwinyi Kazimoto ameendelea kuongeza
idadi ya wachezaji wa Tanzania wanaokwenda kucheza soka la kulipwa na
kurejea nchini kuendelea kucheza timu za ligi kuu soka Tanzania bara.
Kiungo
huyo ambaye alikuwa anaichezea klabu ya Al Markhiya inayoshiriki ligi
kuu ya Qatar tangu mwaka 2013 akitokea klabu ya Simba amerejea tena
msimbazi na kusaini mkataba wa miaka miwili mbele ya Rais wa Simba,
Evans Elieza Aveva.
0 comments:
Post a Comment