Klabu ya
Simba kwa kushirikiana na Jumia wamezindua huduma ya kununua jezi za Simba 2015
– 2016 kupitia duka la mtandao la Jumia www.jumia.co.tz
. Dhumuni la huduma hii ni kuwapatia wapenzi wa klabu ya Simba njia bora ya
kuweza kununua jezi popote walipo Tanzania.
Kupitia
mtandao imara na wenye uzoefu wa Jumia, klabu ya Simba inapanga kuongeza
upatikanaji wa vifaa vyake ya michezo nchi nzima. Mkataba huu utaongeza
usambazaji wa vifaa vya michezo vya klabu ya Simba. “Ukuaji kasi wa upatikanaji
wa internet (mtandao) klabu ya Simba inafahamu umuhimu wa kuvifanya vifaa vyake
vya michezo kuweza kupatikana kiurahisi kwa wateja wake, hivyo leo tunajivunia
kuzindua huduma hii ya Jumia – Simba Online Shop kwa ajili ya kutumia mtandao
wa Jumia kuwezesha wapenzi wa Simba popote walipo kuweza kununua mavazi na
bidhaa az Simba kiurahisi na kwa bei nafuu”. Alisema Ras wa Simba Evans Aveva
Maneja wa
Jumia nchini Tanzania Jean –Philippe Boul aliongeza kwa kusema “uzinduzi wa
jezi za mpira wa miguu siku zote ni tukio muhimu kwenye maisha ya klabu maarufu
na inayopendwa kama Simba. Katika msimu wa 2015 – 2016 klabu ya Simba imeamua
kuwa wabunifu kwa kutoa fursa kwa wapenzi wake kununua jezi za msimu 2015 –
2016 kupitia njia ya mtandao. Tunajivunia sana kwa Rais wa Simba Evans Aveva
kutuchagua Jumia kwa kazi hii. Kupitia huu umoja wetu wa Simba na Jumia
tumeamua kutoa ofa kwa wanachama na wapenzi wa Simba kuagiza jezi kuanzia
Jumatatu tarehe 27 – 7 – 2015 mpaka Alhamisi 31 – 7 – 2015 kupitia www.jumia.co.tz kabla ya kuanza rasmi kwa
mauzo ya kimtandao kupitia Jumia na kuanzwa kuuzwa rasmi kwa rejareja”.
“Tunawahamasisha
wapenzi wa Simab popote walipo Tanzania kuagiza jezi kupitia www.jumia.co.tz kuona urahisi katika kufanya
manunuzi. Popote walipo wapenzi wa Simba wanaeza kuagiza jezi kupitia touti ya
jumia na kuletewa mzigo wako mpka mlangoni. Jumia pia inatoa njia tofauti za
ulipia kama ile kuweza kulipia pindi mzigo wakoutakapofika au kufanya malipo
kwa njia za kipesa kupitia simu za mkononi. Kuanzia jumatatu 27 – 7 – 2015
wapenzi wa Simba watapatafursa ya kuagiza jezi kupitia www.jumia.co.tz”. Aliongeza Maneja wa Jumia
nchini Tanzania Jean –Philippe Boul.
Kuzungumzia mapinduzi haya makubwa katika usambazaji wa vifaa ya michezo ya klabu ya Simba Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya EAGgroup Limited Imani Kajula ambao ni washauri na watekelezaji wa masuala ya kibiashara wa klabu ya Simba alisema “kwa mapinduzi haya makubwa yataiwezesha klabu ya Simba kuongezamapato yake pia kudhibiti bidhaa feki, kupitia Jumia Online Shops (duka la mtandao la Jumia) wapenzi wa Simba watanunua bidhaa za Simba kupitia washirika halali wa uuzaji wa bidhaa za Simba Tanzania.
0 comments:
Post a Comment