MAWASILIANO

Phone. - +255 (717) 300 260 - +255 (787) 300 260

HABARI YA MUJINI

HABARI YA MUJINI
watu wa mpira

Golikipa kutoka Ivory Coast kufanyiwa majaribio


Golikipa kutoka Ivory Coast kufanyiwa majaribio
Katika kujenga kikosi cha Simba na kuyafanyia kazi mapendekezo ya Kocha mkuu wa Simba Dylan Kerr, klabu ya Simba inamfanyia majaribio golikipa Vincent Angban kutoka Ivory Coast.Angban ataungana na kikosi cha Simba kilichopo visiwani Zanzibar kwa ajili ya kufanyiwa majaribio kabla ya kujiunga rasmi na klabu ya Simba.
Simbasports.co.tz iliongea na kaimu katibu mkuu wa Simba Collin Frisch ambaye alisema kuwa wameamua kumfanyia majaribio golikipa Vincent Angban baada ya kocha mkuu Dylan Kerr pamoja na Kocha wa makipa Abdul Idd Salim kuomba uongozi wa Simba kuongeza nguvu kwenye idara ya magolikipa.
Vincent Angban amezaliwa tarehe 2 – 2 – 1990 Anyama Ivory Coast. Mwaka 2005 alikwakilisha timu ya Ivory Coast katika michuano ya kombe la Afrika chini ya miaka 20 nchini Benin na pia mwaka 2008 aliwakilisha Taifa la Ivory Coast katika michuano ya Olympics.
Simbasports.co.tz itaendelea kukuletea maendelea ya golikipa Vincent Angban katika kambi ya Simba iliopo visiwani Zanzibar. SIMBA NGUVU MOJA
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment