MAWASILIANO

Phone. - +255 (717) 300 260 - +255 (787) 300 260

HABARI YA MUJINI

HABARI YA MUJINI
watu wa mpira

YAYA TOURE ANALIPWA KWA WIKI, RAIS KIKWETE ANACHUKUA MWAKA MZIMA, SOKA NI AJIRA KUBWA KULIKO…


Na Ben Shija,DSM.
MARAIS wa Afrika ni kati ya wanaolipwa zaidi ikiwezekana hata kuliko wale wa Ulaya. Lakini imekuwa ikielezwa kwamba wana posho zao za pembeni zinazowafanya wapate fedha zaidi.

Yote yanawezekana na mfano mzuri ni ule wa Rais Teodoro Nguema wa Equatorial Guinea aitwaye Obiang’ Mangue aliyetumia hadi dola milioni 315 kwa manunuzi ya samani na vitu vingine vya kifahari kuanzia mwaka 2004 na 2011.
Mangue ni waziri, kwa mwaka mshahara wake ni dola 100,000 (zaidi ya Sh milioni 210). Hivyo mshahara unaweza usiwe kitu kwa marais wa Afrika.
Lakini kama utazungumzia kila kitu kiende kwa utaratibu, halafu kama kweli wanaotaka urais inakuwa ni kwa ajili ya kufuata maslahi, basi ingekuwa ni bora wote wakacheza mpira na kutafuta mafanikio ya kukipiga Ulaya ambako wangelipwa zaidi.
 
RAIS KIKWETE
Wanasoka wa Afrika wanaocheza barani Ulaya wanaonekana kulipwa fedha nyingi kuliko marais wa nchi zao.
Pamoja na kuwa nchi yake ni ndogo, lakini Rais wa Cameroon, Paul Biya, ndiye anaongoza kwa kulipwa zaidi kuliko marais wengine wote wa Afrika kwa kuwa kwa mwaka anachukua dola 630,000 (zaidi ya Sh bilioni 1.3).
Hiyo inashangaza kwa kuwa Biya anamshinda Jacob Zuma wa Afrika Kusini kwa mshahara licha ya kwamba nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika inaizidi Cameroon mara 10 kiuchumi.
 
RAIS BIYA
Kwa yeye Biya anachukua mshahara mara 229 dhidi ya wananchi wa kawaida, hasa waajiriwa wa serikalini. Huku Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf akiwa anachukua mara 113 zaidi ya wananchi wa kawaida.
Usishangae, Rais wa Somalia, Sheikh Hassan Mohamoud anayechukua dola 120,000 kwa mwaka pia ni kati ya marais wanaolipwa vizuri.
Kwa mujibu wa Daily Mail na Dail Nation, inaonyesha Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete anachukua dola 192,000 (Sh milioni 405) kwa mwaka na kumfanya ashike nafasi ya nne kwa marais wanaolipwa vizuri Afrika.
Kikwete anafuatiwa na Obiang’ Mangue wa Guinea ya Ikweta halafu Uhuru Kenyatta wa Kenya anayechukua 132,000 na marais hawa wawili wa Afrika Mashariki ndiyo pekee walio katika 10 bora ya wanaolipwa vizuri zaidi.
Kinachovutia zaidi ni kwamba ni hivi, pamoja na ukubwa wa marais hao, lakini wachezaji wanaokipiga Ulaya katika Ligi Kuu za England, Italia, Hispania na Ujerumani, wanalipwa vizuri zaidi ya wakubwa hao wa nchi.
 
KOLO TOURE NA WACHEZAJI WENGINE WA IVORY COAST
Mfano Rais wa Ivory Coast, Allasane Ouattara anachukua mshahara wa dola 100,000 kwa mwaka, fedha ambazo Yaya Toure wa Manchester City anazipata kwa wiki tena mara tatu yake na ushee kwa kuwa analipwa pauni 240,0000 kwa wiki ambayo ni zaidi ya Sh milioni 789.
 Kwa mwaka Toure anaingiza pauni milioni 13, fedha ambazo ni zaidi ya mara 24 anazolipwa rais wake ambaye ndiye kiongozi wake wa nchi.
Kama utazungumzia kwa kiongozi wetu wa nchi, Toure anachukua zaidi ya mara 18 ya fedha anazolipwa kwa mwaka.
Hii inaonyesha kiasi gani mchezo wa soka ambao hauhitaji mtu kupata elimu ya chuo kikuu, unaweza kukuletea mafanikio makubwa.
Kipaji ndiyo, lakini juhudi kuu pamoja na nia ya kutimiza kitu kikubwa ndiyo sehemu ya mafanikio makubwa.
Mshambuliaji wa TP Mazembe, Mbwana Samatta, analipwa dola 120,000 kwa mwaka kupitia mshahara wake wa mwezi. Utaona tofauti ya Samatta na Rais Kikwete ni dola 72,000. Fedha ambazo baada ya muda mchache ujao kama Samatta atapata nafasi ya kucheza Ulaya, basi atazipata na zaidi.
Mifano hiyo ya wanachoingiza marais wa Afrika na wachezaji wanaocheza Ulaya kwa wao kuonekana wana fedha nyingi zaidi inaweza kuwa changamoto kubwa kwa viongozi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.
RAIS ZUMA
Wanapaswa kujua michezo na hasa soka, inalipa na inasaidia kupatikana kwa ajira ya uhakika. Kwani hata kama wachezaji hawatalipwa kama akina Yaya, Didier Drogba na Samuel Eto’o lakini wana nafasi ya kupata ajira kubwa kuliko mawaziri au mabosi wa makampuni makubwa ya serikali, pia yale ya binafsi.
Tanzania ihame kutoka kuufanya mchezo wa soka kama sehemu ya kujiburudisha au watu wengine kupata nafasi ya kuwatania wengine baada ya kufunga, badala yake uwe kwenye programu za nchi kuuendeleza na kuufanya uisaidie nchi kuwasaidia vijana wajiajiri kwa kuwa si kila mmoja atasoma na kupata digrii.
                            MSHAHARA WA   WIKI             MWAKA
1        Yaya Toure (Man City)                  £240,000       £13.5m
2       Asamoah Gyan (Al-Ain)                 £120,00          £7.5m
3       Emmanuel Adebayor (Spurs)         £101,000         £5.4m
4        Samuel Etó’o (Everton)                 £80,000           £4.2m
5       Didier Drogba (Chelsea)                 £75,000           £3.8m
6       Mikel John Obi (Chelsea)               £75,000            £3.8m
7       Michael Essien (AC Milan)            £60,000             £2.9m
8       Christopher Samba (Dynamo)        £60,000              £2.9m
9       Kolo Toure (Liverpool)                   £60,000            £2.9m
10     Seydou Keita (AS Roma)                £55,000           £2.9m
    MISHAHARA YA MARAISI             MWAKA
1.   Paul Biya (Cameroon)                        $ 630,000
2.   King Mohammed (Morocco)              $ 480,000
3.   Jacob Zuma (Afrika Kusini)               $ 272,000
4.   Jakaya Kikwete                                  $192,000
5.   Abdelaziz Bouteflika (Algeria)          $168,000
6.   Obiang’ Mangue (E. Guinea)             $150,000
7.   Uhuru Kenya (Kenya)                        $132,000
8.   Ikililou Dhoinine (Comoro)                $115,000
9.   Denis Sassou Nguesso (Congo)         $110,000
10.                Hage Geingob (Namibia)    $110,000
11.                Roberto Mugabe (Zimbabwe) $108,000
12.                Ameena Gurib (Mauritius)   $104,000
13.                Allasane Ouattara (Ivory Coast) $100,000
14.                llen Johnson Sirleaf (Liberia) $90,000
15.                Paul Kagame (Rwanda)        $85,000

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment