Nimepitia Ukurasa Masau Bwire, msemaji machachari wa Ruvu Shooting na kukutana na Posti ya asubuhi akisema:
"KMKM imefungwa karibu mechi zote ilizocheza Kagame, sijui
kwa nini! Nadhani ni bahati tu, uwezo wa kucheza mpira upo.
Usishangae leo bahati wakashushiwa hawa jamaa wakafanya kweli
wakaleta shida mitaa ya Jangwani!
Naomba hilo lisitokee, waendelee tu kukosa bahati ili
Jangwani waneemeke.
Siyo kwamba siwapendi hawa Wazanzibar, nawapenda sana, ni
Watanzania wenzangu, ni kwa sababu pointi tatu kati yake na Jangwani hazina
faida kwake kama ambavyo zina faida Jangwani.
Nawaombea Msimbazi wafanikishe usajili wa Olunga, wasajili
na wengine mahiri ili ligi kuu ya msimu huu wafanye vema, wapate nafasi
kushiriki mashindano ya kitataifa.
Kukosekana kwa Simba msimu huu katika mashindano ya Kagame,
msisimko umekuwa kiduchu!
Katika mashindano yoyote hasa yanayofanyika nchini huwa na
msisimko mkubwa mno yanaposhirikisha Simba na Yanga. Kukosekana kwa timu
mojawapo, mashindano hudolola!
Simba oyeeeeer.....
Yanga mbele daima...."
0 comments:
Post a Comment